Home Kitaifa Umoja wa Makanisa waasa ushirikiano

Umoja wa Makanisa waasa ushirikiano

Na Neema Kandoro Mwanza

UMOJA wa Makanisa ya Kipentekoste Jijini Mwanza umewataka waumini wa madhehebu hayo kudumisha ushirikiano baina yao Ili kuwezesha utulivu kwenye jamii ya watanzania.

Wito huo umetolewa Leo jijini Mwanza katika uchaguzi wa viongozi wa umoja huo ambapo Mchungaji Josephat Magumba alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na Padri George Nzungu Makamu Mwenyekiti na Mchungaji Abel Lugayila kuwa Katibu Mkuu.

Mchungaji Magumba alisema siku zote umoja ni nguvu,Utengano ni Uzaifu hivyo uongozi uliochaguliwa utafanya kazi kubwa ya kuunganisha waumini wote wa Kipentekoste waweze kuwa na sauti ya pamoja itayowawafanya wasaidiane katika masuala yote ya kijamii na kiimani.

Naye Makamu Mwenyekiti Padri Nzungu alisema kuwa watafanya kazi kwa juhudi na maarifa Ili kuimarisha misingi ya imani ya wakiristo kwa watanzania Ili kuwezesha jamii kuepuka aina yote ya upotoshwaji kwa kutumia mwamvuli wa Imani hiyo.

Alisema kuibuka kwa mahubiri ambayo yanasababisha hofu na taharuki kwa jamii haitafanywa na makanisa yaliyo katika muungano wao kwani yanaamini katika ukweli wa maadili yaliyo kwenye kitabu kitakatifu Cha biblia.

Mahubiri kama yaliyotendwa na Mackenzi wa Kenya na kupelekea watu kupoteza maisha kwa kutumia maarifa duni juu ya Imani ya watu hao haina nafasi kwetu”alisema Padri Nzungu.
Katibu wa Umoja huo Mchungaji Abel Lugayila alisema katika Kipindi chao Cha uongozi watahakikisha kuwa kunakuwepo mfuko ambao utawezesha maendeleo na kusaidia pale panapotokea changamoto.

Alisema wataandaa mpango kazi maalumu kuhakikisha kuwa wanafikia mafanikio katika malengo ambayo umoja huo umekusudia.

Naye Mtumishi wa Kanisa CAG Uzima tele Nabii Samweli Kisinza alipongeza uchaguzi huo akisema wamechaguliwa watu sahihi watakaowezesha umoja huo kufikia malengo yake kwenye umoja huo wa Kipentekoste.

Aliomba viongozi hao kushirikiana na serikali ya mkoa katika utendaji kazi zao Ili kuwezesha misingi ya amani na utulivu kutamalaki jijini Mwanza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!