Home Kitaifa UMMY: TUTAJENGA MASOKO YA KISASA TANGA WANANCHI MSIHOFU

UMMY: TUTAJENGA MASOKO YA KISASA TANGA WANANCHI MSIHOFU

NA BONIFACE GIDEON, TANGA

Mbunge wa Jimbo la Tanga ambaye pia ni Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Ujenzi na ukarabatI wa Masoko makubwa Jijini Tanga utaanza muda wote kuanzia Sasa hivyo amewaomba Wananchi na Wafanyabiashara kuondoa hofu kuwa Masoko ya Jiji Hilo yamesahaulika.

Ummy alibainisha hayo mwishoni mwa wiki Wakati akihotubia Wananchi wa kata ya Makorora kwenye Mkutano wa hadhara, “Wananchi wangu msiwe na hofu kabisa kuhusu Masoko yetu ,Soko letu la Makorora Sh.6 Bil.zimeshaletwa na hivi karibuni Ujenzi utaanza rasmi na tutakuwa na soko la kisasa kabisa lakini pia tunayo Masoko mengine ya Mgandini ambalo linahitaji zaidi ya Bil.16 ili kukamilisha Ujenzi na Sasa hivi tunatafuta Wadau lakini soko la Mlango wa Chuma pesa ipo Tayari zaidi ya mil.200 na ukarabatI utaanza Wakati wowote na hii itawasaidia Wafanyabiashara na Wananchi kupata huduma kwa urahisi zaidi” Alisisitiza Ummy

Wakati huo huo Waziri Ummy aliwatoa hofu wanufaika mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri Nchini kwaajili ya Vijana, akinamama na Watu Wenye Ulemavu kuwa Serikali ipo kwenye marekebisho ya njia Bora zaidi za upataji wa mikopo ya Halmashauri ,

Naomba niwatoe hofu juu ya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri,msihofu mwezi wa 7 itaanza kutolewa kwa utaratibu mzuri zaidi ya awali” Alisema Waziri Ummy

Kwa upande wake mustahiki meya wa Jiji la Tanga Abdul Rahman Shillow Aliwataka Wananchi kupuuzia Taarifa zilizotolewa hivi karibuni na Viongozi wa vyama vya siasa Jijini Tanga kuwa Halmashauri hiyo imetafuna fedha za ununuzi wa magari ya Taka,

Hivi karibuni Kuna wanasiasa walitoa Taarifa za kupotosha kwenye majukwaa kuwa Halmashauri yetu Kuna Watumishi wametafuna hela za magari ya Taka, naomba niwaambie magari yapo na mwenge utazindua” Alisema Shillow

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!