Home Afya UMMY: HAKUNA WAGONJWA WAPYA WALA VIFO VYA WATU WALIOPATIKANA NA UGONJWA WA...

UMMY: HAKUNA WAGONJWA WAPYA WALA VIFO VYA WATU WALIOPATIKANA NA UGONJWA WA MARBURG

Na Magrethy Katengu

Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema muenendo wa Ugonjwa wa MARBURG uliogundulika hivi karibuni Wilaya ya Bukoba,Vijijini,Mkoani Kagera hakujapatikana Wagonjwa wapya wala vifo na tayari mgonjwa mmoja amesharuhisiwa akiwa na afya njema .

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema hadi kufikia Aprili 2023 jumla ya watu 212 waliotangamana na Wagonjwa kati ya watu 35 wamemaliza siku 21 za uangalizi za uangalizi bila kuonesha dalili zozote za ugonjwa huo hivyo wameruhusiwa kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na kuungana na familia .

Jumla ya visa 8 na kati yao watu 5 wamefariki ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa hatujapata Wagonjwa wapya wala vifo ninayo furaha kubwa kuwajulisha kues leo tumemruhusu mgonjwa mmoja mwanaume mwenye umri wa miaka 26 akiwa na afya njema“amesema Ummy

Sanjari na hayo aliendelea kufanya kuwa Wagonjwa wawili walilazwa wanaendelea vizuri na matibabu katika vituo maalum vilivyoandaliwa hivyo serikali inatoa Shumrani za pekee Kwa Wataalamu wote wa afya waliokuwa mstari wa mbele kutoa huduma bora kwa Wagonjwa usiku na mchana kuhakikisha afya zao zinatengamaa

Aidha Sekali bado inahimiza wananchi wote na hasa wa Mkoa wa Kagera kuendelea kuchukua tahadhari kudhibiti ugonjwa na kuzuia maambukizi mpya katika Jamii na endapo kutakuwa na mtu yeyote kwenye Jamii mwenye dalili za homa kali ikiwemo kutapika ,kuharisha ,kutokwa damu na mwili kuishiwa nguvu atoe taarifa haraka kwa kupiga simu 199 bila gharama zozote Ili apatiwe msaada wa haraka

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!