Home Kitaifa (UMKI)WAJIPAMBANUA KUUNGA JUHUDI ZA SERIKALI UJENZI WA MAENDELEO KIJIJI KIKUKWE MISSENYI.

(UMKI)WAJIPAMBANUA KUUNGA JUHUDI ZA SERIKALI UJENZI WA MAENDELEO KIJIJI KIKUKWE MISSENYI.

Na Theophilida Felician Kagera.

Wanaumoja wa Maendeleo Kijiji cha Kikukwe UMKI wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera wapiga hatua katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za ujenzi wa Maendeleo ya Kijiji hicho cha Kikukwe kilichopo kata Kanyigo.

Yameelezwa hayo na viongozi wa umoja huo kwenye Sherehe za umoja huo zilizofanyika shule ya Sekondari ya Kikukwe ambapo katibu wake Magreth Domisian Kyai ametoa ripoti ya yatokanayo na utekelezaji na malengo ya kazi zao kwa mwaka wa 2022/ 2023.

Amezitaja baadhi Shughuli kuwa ni ujenzi wa kituo cha afya Kanyigo, kuweka maji shule ya sekondari Kikukwe, kuanzisha shamba darasa la parachichi hekari 2 na shamba darasa la vanilla, kiwango cha hekari 10 kwenye uwekezaji.

Amefafanua kuwa katika shamba darasa la vanilla na migomba mazao yake yaliyopandwa kwa gharama ya sh 730, 000.00 yanaendelea vizuri.

Shughuli nyingine nipamoja na ushiriki wa ujenzi unaondelea wa bweni la shule ya sekondari Kikukwe, kushiriki michezo kupitia ligi za kata ya Kanyigo na Kashenye kwa sikukuu ya nane nane , ikiwa ni sambamba na kupokea wanafunzi 5 kutoka chuo cha Butiama kwa ajili ya mafunzo kwa shule ya sekondari Kikukwe hivyo UMKI waligharamia mahitaji ya chakula malazi kwa Sh 1,520,000.00. ndani ya kipindi cha miezi 3.

Katibu huyo pia ameongeza kusema kwamba umoja huo umeundwa na washiriki mbalimbali 172 wanaoishi katika Kijiji hicho na wengine wapo nje ya mkoa na nje ya nchi.

Mwenyekiti wa umoja Eng, Godifrey Mugini awali akielezea malengo ya UMKI amesema kuwa malengo makubwa ni kuinua maendeleo ya Kijiji kiuchumi kwakushirikiana na serikali kwani kwa muda wa miaka mitatu tangu kuanza kwake tayari wamezigusa sekta za elimu, afya, maji, kilimo, ufugaji na miundo mbinu kadha wa kadha.

Licha ya hayo Mwenyekiti Godifrey amezitaja changamoto baadhi ikiwemo ya barabara ya kutoka kata Gera kuelekea mpakani mwa nchi jirani Uganda yenye kiwango cha changarawe kuwa nichangamoto kwa wananchi hususani nyakati za mvua inapitika kwa shida hivyo ameiomba serikali kufanya jitihada za kuijenga kwa kiwango cha lami ili kuwanusuru wananchi na adha hiyo.

Walter Nyahoza ni diwani wa kata hiyo ya Kanyigo ameupongeza umoja huo kwa jinsi unavyoendelea kusimama imara nakusaidia kuyajenga maendeleo ya Kikukwe na Kanyigo kwa ujumla.

Mgeni rasmi akiwa ni katibu tawala wa wilaya Missenyi Mwanaid M. Manguro kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa Kagera amewapongeza UMKI nakuwashukuru kwa kuwa bega kwa bega na serikali katika kuunga mkono ujenzi wa miradi ya maendeleo kijijini humo.

Kabla sijaja hapa kwenye jukwaa nimekagua miradi yenu ukiwemo huu wa ujenzi wa bweni la wanafunzi hongereni sana sana ninyi ni Kijiji cha kuigwa ni kijiji cha mfano wengine huanzisha umoja kama huu lakini wengi wao hushindwa na kuishia njiani ila nyie mkoa vizuri simameni hivyohivyo” amesema Katibu tawala Mwanaid.

Amewahidi kuwa serikali ikatuwa na umoja huo sambamba kwa kila jambo hususani katika kushughulikia changamoto walizozitaja ikiwemo ya barabara na nyinginezo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!