Home Kitaifa ULEGA AONGOZA VIONGOZI WA HALMSHAURI YA MKURANGA KUTOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA...

ULEGA AONGOZA VIONGOZI WA HALMSHAURI YA MKURANGA KUTOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI NA KIBITI

Na Scolastica Msewa, Rufiji
Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mheshimiwa Abdallah Ulega ameongoza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kutoa msaada wa vyakula tani nne yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5 na boti itakayosaidia usafiri na shughuli za kipindi cha athari za mafuriko kwa waathirika hao wa Wilaya ya Kibiti na Rufiji.

Akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Mkuranga wakati alipofika kutembelea na kukagua athari za mafuriko ya Wilaya ya Rufiji Mheshimiwa Ulega alisema wamekuja wilayani humo ikiwa ni kwasababu ya ujirani mwema uliopo Kati ya Wilaya ya Mkuranga na Wilaya za Kibiti na Rufiji wameona wajekutoa msaada wao wa hali na Mali kwa waathirika Kata 17 za Wilaya hizo.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga wamewiwa waende wakawashike mkono kwa chakula hicho cha tani nne za unga wa sembe na dona na mafuta ya kupikia ilikuwanusuru waathirika hao wa mafuriko ya Wilaya za Kibiti na Rufiji.

“Mimi na wenzangu tumejipanga kukabithi boti itakayosaidia shughuli za uokozi na usambazaji wa chakula na huduma kwa waathirika hao wa mafuriko ya Wilaya za Kibiti na Rufiji” alisema Mheshimiwa Ulega.

Aidha kwa upande wa wizara ya uvuvi na mifugo imeagizwa na Mamlaka za juu iendelee kufanya tathimini hivyo Wataalamu wa wizara hiyo kwa kushirikiana na Wataalamu wa Wilaya hizo kwa kushirikiana na Wataalamu wa wizara zingine kufika katika Wilaya hizo na kupata tathimini ya miundombinu ilivyoathirika katika Wilaya hizo.

Hatahivyo ameahidi kutoa ushirikiano wa bega kwa bega kuwasaidia Wilaya hiyo na kuwataka Wananchi kuendelea kuchukua tafadhali za kiusalama kipindi hiki cha mafuriko.

Naye Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa akipokea misaada hiyo ameshukuru kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kupeleka msaada huo na kusema kiongozi Bora ni yule anayejali Wananchi wakati wa shida zao na kutafuta utatuzi.

Hata hivyo, Mheshimiwa Mchengerwa amekabidhi ahadi yake ya shillingi milioni 50 kwa Mkuu wa wilaya Meja Edward Gowele kwaajili ya kununua mbegu za kilimo kwa Waathirika wa mafuriko hayo.

Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge ameshukuru kwa misaada mbalimbali inayoendelea kutolewa na kuahidi kusimamia misaada hiyo iwafikie walengwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!