Home Kitaifa ULEGA AKABIDHI BOTI YA THAMANI YA MILIONI 42 RUFIJI

ULEGA AKABIDHI BOTI YA THAMANI YA MILIONI 42 RUFIJI

Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amepokea ahadi ya Msaada wa boti yenye mashine kutoka kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega aliyewakilishwa na Katibu wa Siasa na uenezi wa CCM wilaya ya Mkuranga Omari Kisatu yenye thamani ya zaidi ya shillingi milioni 42 kwaajili ya shughuli mbalimbali za usafiri na uokozi wa Waathirika wa mafuriko yanayoendelea katika mto Rufiji kwa Wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani.

Kunenge ameshukuru kwa msaada huo nakusema Boti hiyo itasaidia katika kipindi hiki cha mafuriko kwa Wilaya za Kibiti na Rufiji.

Boti hii itatusaidia sio tu kwa Wilaya ya Rufiji bali tutaitumia pale ambapo tutaona Kuna mahitaji zaidi kwasasa bado Kuna sehemu Kuna Wananchi wanahitaji kuokolewa ili waletwe sehemu salama zaidi” alisema Kunenge na kukabithi boti hiyo kwa Kamanda wa zimamoto mkoa wa Pwani Jennifer Shirima.

Alikabidhi Boti hiyo Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Mkuranga Omary Kisatu kwaniaba ya Ulega alisema boti hiyo imeletwa kwaajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za maafa yaliyojitokeza kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini kote.

Wiki Moja iliyopita Ulega alifika Wilayani Rufiji kuleta michango mingine kwa waathirika hao wa mafuriko lakini aliahidi kuleta Boti hiyo kwaajili ya kusaidia changamoto zilizokitokeza katika Wilaya hizo

Alisema mchango huo binafsi ni mwanzo ya kwamba anaendelea kujipanga zaidi kusaidia zaidi kwa kadri Mwenyezi Mungu atakavyomuwezesha atasaidia.

Naye Kamanda wa zimamoto mkoa wa Pwani Jennifer Shirima alishukuru kwa msaada huo na kuomba Wadau wasaidie zaidi upatikanaji wa Boti kwani mahitaji ni makubwa kwani kulikuwa na boti tatu zinazotumika katika uokoaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!