Na Mercy Maimu
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge viwanda biashara na Mazingira David Mwakiposa Kihenzile amesema lengo la kuanzishwa kwa kituo Cha Misugusugu ni kuhakika magari,dira za maji na dira za umeme ili kuepusha utoaji wa mita za maji zisizokuwa na ubora kwa wateja.
Ameyasema haya Leo akiwa kwenye ziara katika kituo Cha Misugusugu ambapo kituo kwenye kuhakiki magari,magari yanayobeba mafuta na dira za maji zinazotumika katika matumizi ya majumbani na viwandani.Dira za umeme zinazotumika majumbani na viwandani
“Tumepta nafasi ya kwenda wanapohakiki mita za maji na za umeme lengo lake ni kuepusha kutoa mita ya maji ambayo haina ubora na viwango vinavyohitajika.
Naye Naibu Waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara Mh Exaud Kigahe ameitaka Taasisi za uwekezaji na viwanda kupitia kituo Cha Misugusugu kutumia vizuri na kuhakiki na kuendeleza miundombinu sahihi kupitia kituo hicho ni mfano Bora Afrika Mashariki
“Kazi kubwa ya wakala wa vipimo ni kumlinda mlaji na mtoa huduma.Mfano dira za umeme zikihakikiwa Tanesco hawezi kuibuwa ikiwa Dira za umeme zinatoa taarifa sahihi za umeme unaopita kwenda kwa watumiaja”.
Aidha amesema serikali inahakikisha inatoa huduma iliyobora kupitia tà asisi zao ikiwemo wakala wa vipimo kushauriana na Serikali katika kuongeza bajeti na kuhakikisha matumizi sahihi ya fedha zinazokusanywa zinatumika vizuri.
“Kamati ya Bunge ya kudumu Wana nafasi kubwa kuelewa nini kama Serikali kupitia tà asisi zetu,na Leo wamepitia wameona pamoja na changamoto walizonazo wanaweza kutushauri vizuriii,kutusaidia kuongeza bajeti na kuhakikisha matumizi sahihi ya fedha zinazokusanywa kama Kodi kwenye huduma hii kwa wateja. Fedha hizo ni za serikali hivyo kuzitaka Taasisi kutumia fedha hizo vizuri na kuhakiki na kuendeleza miundombinu sahihi” amesema Kigahe
Kwa upande wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Stella Kahwa ameishukuru Kamati ya Bunge viwanda, biashara na Mazingira kutembelea kituo Cha Misugusugu na kupokea maoni na ushauri kuhusiana na uboreshaji na uendelezaji wa kituo hicho