Home Kitaifa UJENZI WA MAABARA TATU ZA MASOMO YA SAYANSI JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI...

UJENZI WA MAABARA TATU ZA MASOMO YA SAYANSI JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI WASHIKA KASI

Na Shomari Binda-Musoma

UJENZI wa maabara 3 za masomo ya sayansi kwenye shule za sekondari jimbo la Musoma vijijini ili kuwafanya wanafunzi kusoma masomo hayo.

Kasi hiyo imefanya kutolewa pongezi na kamati ya utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi wa CCM mkoa wa Mara iliyofanya ziara kwenye jimbo hilo jana Septemba 3

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mara Julias Kambarage Masubo aliyeongoza kamati hiyo ametoa pongezi kwa jitihada za mbunge wa jimbo hilo Profesa Sospeter Muhongo kwa kushirikiana na wananchi kwenye ujenzi huo.

Amesema masomo ya sayansi yana umuhimu mkubwa katika soko la ajira hivyo maabara hizo zitawafanya wanafunzi kusoma kwa vitendo.

Masubo amesema jitihada za mbunge Muhongo na wananchi zinaonekana na kuwataka viongozi wengine kwenye maeneo yao kufanya hivyo.

Amesema jmbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 kwa sasa lina sekondari 26 za Kata na 2 za madhehebu ya dini huku ujenzi wa sekondari mpya 11 unaendelea kwenye baadhi ya Kata.

“Ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi (physics, chemistry & biology laboratories) unaendelea vizuri kwa sekondari zote za Kata za jimbo la Musoma vijijini.

“Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Muhongo na wananchi wanaunga mkono juhudi za serikali kwenye kuchangia lazima tupongeze kwa hili”,amesema

Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mara wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa walitembelea Kata ya Nyakatende yenye sekondari mbili za Nyakatende na Kigera na kushududia maendeleo mazuri ya miradi ya ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi kwa kila sekondari ya Kata

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!