Na Shomari Binda – Musoma
Jimbo la Musoma vijijini limeamua kutatua tatizo sugu la ukosefu wa maabara za masomo ya sayansi kwenye sekondari zake za kata kabla ya kuanza msimu ujao wa masomo.
Lengo kuu ni kila sekondari ya Kata ipate maabara nzuri na za kisasa za masomo matatu ya sayansi physics, chemistry na biology labs.
Wachangiaji wakuu wa mradi huu wa ujenzi wa maabara ni wanavijiji,serikali kuu,mbunge wa jimbo Profesa Sospeter Muhongo,mfuko wa jimbo pamoja na baadhi ya wazaliwa wa Musoma vijijini
Halmashauri ya Musoma (DC) imeendelea kushauriwa nayo ianze kuchangia mradi huu kwa kutumia mapato yake ya ndani ili kufikia lengo la ukamilishaji wake.
Takwimu za maabara inaonyesha sekondari zenye maabara tatu (3) ni Bugwema, Kiriba
, Ifulifu na Mugango huku Bwai zikitegemea kukamilishwa januari 2024.
Sekondari zenye maabara mbili (2) Bulinga, Kigera ,Nyakatende, Makojo,Nyambono, Nyegina, Rusoli ba Suguti.
Kwa upande wa sekondari zenye maabara moja ni
Bukima, Dan Mapigano (Bugoji), Etaro, Kasoma
pamoja na Mabuimerafuru
Kwa sasa sekondari zizokuwa na maabara hata moja ni Nyegina, Busambara,Mtiro, Murangi, Nyanja, Seka na Tegeruka.
Sekondari za binafsi zimejenga maabara zake ambazo ni Bwasi (Kanisa la Wasabato/SDA)
na Nyegina (Kanisa Katoliki/RC)
Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini profesa Sospeter Muhongo amewakaribisha wadau wa elimu kuendelee kuchangia ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi kwenye sekondari za Kata za Musoma vijijini
Aidha amewakumbusha wadau hao kukumbuka harambee ya ujenzi wa maabara za Etaro sekondari utakaofanyika Ijumaa desemba na kudai sayansi ni kila kitu na kila kitu ni sayansi.