Home Kitaifa UJENZI KITUO CHA AFYA KISIWA CHA RUKUBA MUSOMA VIJIJINI WAKAMILIKA

UJENZI KITUO CHA AFYA KISIWA CHA RUKUBA MUSOMA VIJIJINI WAKAMILIKA

Na Shomari Binda-Musoma

UJENZI wa kituo cha afya katika kisiwa cha Rukuba kilichopo Kata ya Rukuba umekamilika na kutarajiwa kuanza kutoa huduma hivi karibuni.

Kwa sasa wananchi wa kisiwa hicho wanaiomba Tamisemi pamoja na Wizara ya Afya kuwapelekea watumishi pamoja na vifaa tiba ili kutoa huduma.

Kuanza kutoa huduma kwa kituo hicho cha afya kutasaidia kusafirisha wagonjwa mahututi na mama wajawazito kusafirishwa kwa mitumbwi kwenda hospital ya rufaa mjini Musoma.

Kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha afya wakazi wa kisiwa cha Rukuba waliamua kupanua zahanati yao iwe kituo cha afya.

Upanuzi huo ulianza kutekelezwa kwa kutumia michango ya fedha na nguvu kazi za wananchi na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini, Prof. Sospeter Muhongo.

Wakazi wa kisiwa cha Rukuba na viongozi wao wanaishukuru serikali kwa kuwapatia shilingi mulioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Kisiwani hapo.

Majengo 4 na miundombinu yake yaliyokamilika ya mama na mtoto, maabara,upasuaji na ufuaji yamekamilika.

Aidha jengo la OPD litatumika la zahanati wakati jengo jipya likiwa linakamilishwa kwaajili ya kutumiwa kwa wagonjwa wa nje

Wananchi wa kisiwa hicho pamoja na viongozi wao wanaishukuru serikali ya awamu ya 6 chini ya Rsis Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha nyingi kwaajili ya miradi mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!