Home Kitaifa UHAMIAJI WAMNASA MTUHUMIWA WA UHALIFU WA KIMATAIFA

UHAMIAJI WAMNASA MTUHUMIWA WA UHALIFU WA KIMATAIFA

Na Mwandishi Wetu, 06th December 2022

Raia kutoka nchini Irani, Bw.Hamidreza Mohammad Ab Raheh mwenye hati ya kusafiria Nambari H46000576 amekamatwa na kurejeshwa nchini kwake mapema leo hii kwa makosa ya kuishi kinyume na sheria nchini na kupanga mipango ya uhalifu wa kimataifa kwa kushirikiana na waharifu wengine.

Akizungumza na wanahabari, Kamishna wa Uhamiaji, usimamizi na udhibiti wa mipaka nchini CI Samweli K. Mahirane amewaasa watanzania wote kushiriki kikamilifu katika kulinda usalama wa nchi yao ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama katika kutoa taarifa fiche dhidi ya wahalifu.

Aidha, Kamishna Mahirane, ameeleza mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa nchini katika kutoa huduma bora kwa wageni, kukabiliana na wahalifu wa kitaifa na kimataifa, wahamiaji haramu na kipekee katika kushirikiana na Taasisi za kimataifa kama vile Shirika la Umoja wa Mataifa la IOM kuwarejesha wahamiaji haramu makwao.

Katika kipindi cha kuanzia Mwezi Januari 2022 hadi Novemba 2022, kumekuwa na ongezeko kubwa la wageni nchini; Ambapo Jumla ya wageni 1,172,205 waliingia nchini kihalali kwa kufuata taratibu na sheria na wageni 983,183 waliondoka nchini. Aidha, Watanzania 220,423 walirudi nchini wakitokea nchi za nje na 250,540 walitoka nchini kuelekea mataifa mengine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!