Home Kitaifa UHAMIAJI TANGA YATOA ONYO KALI KWA MADALALI WA WAHAMIAJI HARAMU

UHAMIAJI TANGA YATOA ONYO KALI KWA MADALALI WA WAHAMIAJI HARAMU

Na Boniface Gideon,TANGA

JESHI la Uhamiaji Mkoa wa Tanga limewaonya mawakala hasa watanzania wanaoji husisha na mtandao wa kuwaingiza wahamiaji haramu mkoani humo kuacha mara moja tabia hiyo kwani siku zao zinahesabika.

Hatua hiyo inatokana na uwepo wa watanzania ambao wanashiriki kwenye mtandao wa kuwaingiza wahamiaji hao na kuwasafirisha kwenda mikoa mengine hapa nchini na hatimaye kuelekea nchini Afrika Kusini kufanya kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo , Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga Kagimbo Hosea amesema hali ipo shwari isipokuwa bado kumekuwa na wimbi kutokana na baadhi ya Watanzania ambao sio wazalendo wamekuwa wakitumika kwenye mtandao wa kuwaingiza wahamiaji haramu nchini.

Amesema kwamba wao kama idara kwa mkoa wa Tanga hawatakubali kuona hilo linafanyika kwenye mkoa huo huku akieleza kwamba wamejipanga imara kuhakikisha wanakabiliana na vitendo vya namna hiyo .

“Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Tanga tumekuwa tukipambana kila wakati kuhakikisha tunautokomeza mtandao wa wahamiaji haramu lakini kuna mawakala ambao wamekuwa wakitumika kuwaingiza niwaonye waache mara moja kwani hawatasalimika pindi watakapokamatwa kwani tumekuwa tukiendelea kutoa elimu lakini vitendo hivyo bado vinaendelea na mawakala ndio chanzo kikubwa” Alisema.

“Lakini pia ndugu zangu watanzania tuendelee kuwa wazalendo,madhara ya wahamiaji haramu ni makuba sana hivyo nitoe onyo kwa watanzania kuachana na biashara haramu za kusafirisha binadamu” Alisema

Hata hivyo alisema mkakati wa Idara hiyo ni kuhakikisha wanadhibiti vitendo hivyo kwenye mkoa huo kwa kufanya vikao kwenye ngazi ya Kata mbalimbali na kutoa elimu kwenye vyombo vya habari hususani radio ili kudhibiti suala la wahaamiaji haramu.

“Lakini niitake jamii pia kuendelea kuwafichukua kwani madhara wanayoweza kuyapata kutokana na biashara hiyo ni makubwa na hao watu wakiingia wana kuwa kundi kubwa na hivyo kuhatarisha usalama hivyo watanzania tuendelea kutoa taarifa pindi tunapowaona watu wa namna hiyo kwenye maeneo yenu” Alisema

Afisa Uhamiaji huyo amesema kwamba waliondoa kuingia nchini bila visa ili watu waingie kwa utaratibu ambao ni wa kulipa visa limeonekana sio tatizo lakini jambo ambalo limejitokeza Tanzania ni mawakala ambao wapo.

“Tumekuwa tukiwaelimisha kwamba waambie ndugu zao utaratibu wa kuingia Tanzania umebadilika wenyewe wanasema tatizo ni madalali wakifika Kenya wanawakamatwa na kuwaambia Tanzania ni kugumu wawape fedha watawasafirisha na wakikataa wanawanyang’anye kila kitu” alisema

Afisa Uhamiaji huyo amesisitiza kuwa wamegundua madalali wa nje na ndani ya nchini na wamekuwa ni changamoto hivyo wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria ili kukomesha mtandao huo .

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!