Theophilida Felician, Kagera
Ugonjwa wa kipindupindu umelipuka Mkoani Kagera nakusabisha vifo vya watu nne na wengine wa nne wamelazwa Hosptalini wakiendelea kupata matibabu.
Akitoa taarifa ya mlipuko wa gonjwa huo kwa umma kupitia vyombo vya habari ofisini kwake Manispaa ya Bukoba Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe Fatma Mwassa amesema kuwa ugonjwa huo ulioanza kutokea mnamo Tarehe 29 Novemba mwaka huu 2023 Kijiji cha Buchurago Kata Bugorora wilaya ya Missenyi umeua watu wanne, watatu wameruhusiwa na wengine wanne bado wanatibiwa katika Hospitali ya St. Tereza.
Amefafanua kuwa kutokana na mlipuko wa kipindupindu Serikali tayari ipo kazini kuhakikisha jihudi zinafanyika juu ya kuudhibiti kabla hujasababisha maafa zaidi ambapo tayari zimechukuliwa sampuli 18 kwa ajili ya vipimo.
Ametoa msisitizo kwa wananchi juu ya kuchukua tahadhari akiwataka kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima, kutokura chakula kwenye mikusanyiko, safari zisizo za lazima, kunawa mikono, kunywa maji yaliyochemshwa, sambamba nakutoa taarifa haraka kwanye kituo cha afya kilichopo karibu na maeneo yao waonapo mgonjwa mwenye dalili ya kipindu pindu kwani kuendelea kumuhudumia wenyewe nyumbani ni hatari ya kueneza maambukizi.
Ameongeza kwamba tayari yameishatengwa maeneo maalumu yakuwaweka wangonjwa wa kipindupindu.