Na Mercy Maimu
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Ilala imeendelea na utekelezaji wa majukumu yake ambapo imeweka kipaumbele katika usimamizi na Ufuatiliaji wa fedha za miradi ya Maendeleo na kuishirikisha jamii kwenye miradi hiyo kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.
Hayo yamesemwa Leo na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Ilala Pilly Mwakasege wakati akitoa taarifa kwa Umma kupitia vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.
Aidha amesema jumla ya miradi ya Maendeleo miwili yenye jumla ya thamani shilingi Bilioni 5385354000 imekaguliwa katika sekta ya afya ikiwa lengo ni kufuatilia na kujiridhisha kama ubora wa kazi unaendana na thamani ya fedha zilizitolewa endapo kama kuna kasoro yoyote zilizojitokeza ziweze kurekebishwa.
“Mradi wa ujenzi wa ICU na manunuzi ya vifaa katika Hospitali ya Amana vyenye thamani ya Tsh 48000000/=mradi huo ulikqguliwa na kuonekana na mapungufu ya Kuta za jengo Hilo la ICU kupinda(hazijanyooka) na mradi kuendelea kutekeleza nje ya muda. Hatua zinazotarajiwa kuchukuliwa ni pamoja na kufanya kikao kazi na kufanya Ufuatiliaji mpka hatua ya mwisho ili malengo ya serikali yafikiwe kwa kiwango Cha kuridhisha”. amesema Pilly
Amesema pia Ofisi imefanya uchambuzi wa mfumo unaojihusisha na ukusanyaji wa mapato hali inayosababisha upotevu wa mapato katika Soko la Samaki Feri,kupitia uchambuzi huu umeamua kuweka CCTV Camera za kutosha, monitor kwenye ofisi za walinzi ili wawe wanafuatilia usalama wa soko na ukusanyaji wa mapato katika Soko hilo.
“Ofisi imefanya uchambuzi wa mfumo unaojihusisha na taratibu na SHERIA zinazohusu ukusanyaji wa mapato,hali inayosababisha upotevu wa mapato katika Soko la Samaki Feri. Katika uchambuzi huo mianya kadhaa ilibainika ikiwa ni pamoja na kutokuwa na usimamizi mzuri na wa kutosha katika Soko,Ajira za muda kutolewa kwa watoza ushuru ambao pia wanalipwa mishahara midogo.”amesema
Ameongeza kuwa TAKUKURU MKOA wa Ilala imeweka mikakati maalum ya kuhakikisha elimu inaendelea kutolea kwa wananchi,vijana na makundi mbalimbali na mkazo wa utaelekezwa kwenye kudhibiti vitendo vya rushwa katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ili kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa ufanisi na inakamilika Kwa wakati na thamani ya fedha (Value for money) inapatikana.
“Elimu ya mapambano Dhidi ya rushwa inaendelea kutolewa kwa wananchi wote na nguvu kubwa ilielekezwa kwa watumishi na Wadau wote wa Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere (JNIA) ikiwa ni pamoja na Askari wa Uhamiaji kwa lengo la kusisitiza umuhimu wa kutoa huduma Bora kwa abiria na wateja wote wanaohudumiwa JNIA”. amesema Pilly