Na Magrethy Katengu
Chuo kikuu Cha Dodoma UDOM chasema tangu maonyesho yaanze mwitikio ni mzuri kwani wamefanikiwa kudahili wanafunzi zaidi ya 5000 wanahitaji kujiunga na chuo hicho
Akizungumza Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano na Umma UDOM Rose Joseph wakati walipotembelewa Banda lao na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adlof Mkenda katika Maonyesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika Jijini Dar es salaam amesema wanamshukuru Mungu kwani mwitikio wa wazazi na wanafunzi siyo mbaya
“Banda letu ni kubwa tumejipanga kuna wataalamu wa kudahili wanaohitaji kujiunga kila ndaki kwa kuwatolea maelezo kwa kina zaidi mwanafunzi anapoenda kusoma aielewe kozi aliyoichagua kuisoma asijutie baadae pia tunatoa huduma ya afya kwa wazazi na wanafunzi” amesema Rose
Aidha Chuo Kikuu cha Dodoma kinawakaribisha wananchi wote kutembelea Banda lao wanadahili wanafunzi wanaohitaji kujiunga pia wanatoa huduma za afya bure