Home Kitaifa UCHAKAVU WA VYUMBA VIWILI VYA MADARASA UKEREWE WAMGUSA MBUNGE

UCHAKAVU WA VYUMBA VIWILI VYA MADARASA UKEREWE WAMGUSA MBUNGE

Vyumba viwili vya madarasa vinavyotumiwa na wanafunzi wa darasa la tatu na la nne katika shule ya msingi Bulubi wilayani ukerewe mkoani mwanza viko hatarini kubomoka kufuatia uchakavu mkubwa unaovikabili.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Ashery Anthony amesema kuwa, uongozi wa shule umeshindwa kuvifanyia ukarabati vyumba hivyo kutokana na shilingi elfu 15 zinazotolewa na serikali kila mwezi kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya elimu na kutokidhi mahitaji.

Shule ya msingi bulubi kata ya Ilangala wilayani Ukerewe mkoani Mwanza inakabiliwa na uchakavu mkubwa wa miundombinu ya madarasa.

Uchakavu wa mindombinu ya shule hiyo iliyoko kwenye kisiwa cha Bulubi kilichoko kwenye Ziwa Victoria unachangia wanafunzi wa shule hiyo kujifunza kwenye mazingira magumu.

Vyumba viwili vya madarasa viko hatarini kubomoka na hivyo kuhatarisha maisha ya zaidi ya wanafunzi 70 wanaotumia vyumba hivyo.

Mbali na uchakavu, Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa unaotekelezwa na Jamii ya kitongoji cha Bulubi umekwamia kwenye hatua ya msingi baada ya uongozi wa kijiji cha Kamasi kudaiwa kutafuna.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ukerewe Joseph Mkundi ametembelea kisiwa cha Bulubi na kuahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo ikiwemo uchakavu wa miundombinu ya madarasa hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!