Home Kitaifa UBALOZI WA USWISI WASHIRIKIANA NA SHIRIKA LA AMEND TANZANIA KUTOA MAFUNZO KWA...

UBALOZI WA USWISI WASHIRIKIANA NA SHIRIKA LA AMEND TANZANIA KUTOA MAFUNZO KWA MADEREVA BODABODA

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MADEREVA bodaboda 145 katika Jiji la Dodoma- wamepatiwa mafunzo ya usalama barabarani awamu ya pili yalioanza Aprili 15 Aprili na kukamilika Mei 4 mwaka huu.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Uswisi kwa kuahirikiana na Shirika la Amend Tanzania yamehitimishwa kwa madereva bodaboda hao kupatiwa vyeti vya ushiriki.

Akizungumza mbele ya madereva bodaboda pamoja na wadau wengine wa usalama barabarani Naibu Meya wa Jiji la Dodoma aliyekuwa mgeni rasmi Asma Karama amewataka madereva hao kuwa mabalozi kwa bodaboda ambao hawajafikiwa na mafunzo hayo.

“Niwasihi madereva wote waliopokea mafunzo haya kuwa mabalozi wazuri wa usalama barabarani katika maeneo yao kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani,” amesema Naibu Meya Asma.

Awali Simon Kalolo kutoka shirika la Amend Tanzania amesema katika utekelezaji wa mafunzo hayo Shirika la Amend linashirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, viongozi wa Serikali za mitaa na shirika la Msalaba Mwekundu wakati wa kutoa mafunzo hayo.

Pia amesema kuwa kupitia mradi huo hadi sasa, mradi huu wa usalama barabarani kwa vijana umewafikia madereva wa pikipiki 398 jijini Dodoma.

“Madereva waliohudhuria mafunzo haya wamepatiwa vyeti vya ushiriki pamoja na viakisi mwanga vyenye ujumbe wa usalama barabarani.Awamu ya kwanza ya mafunzo haya, madereva 253 kutoka kata za Jiji la Dodoma wamenufaika.”

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!