Home Kitaifa TUTAWASAIDIA KUONDOA VIKWAZO VYA KIBIASHARA – CG MWENDA

TUTAWASAIDIA KUONDOA VIKWAZO VYA KIBIASHARA – CG MWENDA

Kilimanjaro,

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Mwenda amewaahidi wafanyabiasha na watoa huduma mbalimbali nchini kuwa Serikali ipo kwaajili ya kuweka Mazingira mazuri ya kufanyia shughuli zao ili ikusanye mapato bila shida.

Akiwa ziarani mkoani Kilimanjaro kwaajili ya kuwashukuru na kuwasikiliza Walipakodi Kamishna Mkuu Mwenda amesema wafanyabiasha na watoa huduma mbalimbali wanapokutana na changamoto wanapaswa kuzungumza na mamlaka zinazohusika na siyo kukaa kimya.

Amesema iwapo hawatavunja ukimya Serikali haiwezi kujua kama wanakabiliwa na Changamoto zozote badala yake itakuwa ikiwadai Kodi.

Amesema katika ukusanyaji wa mapato biashara kwanza ndiyo mapato yanafuata hivyo jukumu la TRA siyo kukusanya mapato peke yake pia wanawajibika kutazama Mazingira ya biashara ili kuondoa vikwazo.

Kamishna Mkuu Mwenda amesema Ziara anazofanya na kuzungumza na Walipakodi moja kwa moja ni zinalenga kutoa zawadi kwa Walipakodi, Shukrani, Elimu na kusikiliza changamoto zao ili kuwawezesha walipe Kodi kwa hiari.

“Nimekutana na kuzungumza na Walipakodi wengi katika mikoa tofauti, nilichogundua tunapaswa kuwa na ukaribu nao, wakati mwingine kinachokosekana ni taarifa sahihi” amesema Kamishna Mkuu Mwenda.

Baadhi ya Walipakodi mkoani Kilimanjaro ambao wamepata fursa ya kutembelewa na Kamishna Mkuu wa TRA akiwemo Catherine Muhina meneja uendeshaji Kampuni ya Utalii ya Alteza amesema awali kabla ya kutembelewa na Kamishna Mkuu wa TRA alikuwa akijua kuwa TRA ni adui wa mfanyabiashara.

Amesema ujio wa Kamishna Mkuu wa TRA umewaondoa hofu na kuwawezesha kueleza changamoto zao Hali itakayowafanya wajivunie kulipa Kodi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!