Home Kitaifa TUSAIDIANE KULINDA MIUNDOMBINU YA UMEME- MENEJA TANESCO MKOA WA PWANI

TUSAIDIANE KULINDA MIUNDOMBINU YA UMEME- MENEJA TANESCO MKOA WA PWANI

Meneja wa shirika la Umeme Tanzania TANESCO mkoa wa Pwani Eng. Cosmas Mkaka ametoa wito kwa baadhi ya Wananchi mkoa wa Pwani wanaojihusisha na vitendo vya wizi wa miundombinu ya umeme mkoani humo kwani husababisha kukatika kwa umeme na kusababisha hasara kwa shirika hilo la Umeme (TANESCO).

Ametoa wito huo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake mjini Kibaha kuhusu changamoto ya wizi wa miundombinu ya umeme mkoani Pwani Eng. Mkaka amesema wizi huo husababisha baadhi ya maeneo kukatika kwa umeme na kufanya shirika hilo kuingia gharama ya kurudishia miundombinu hiyo kwaajili ya kuwapa Wananchi Umeme.

Ametoa wito kwa Wananchi akiomba ushirikiano wa ulinzi katika miundombinu ya umeme katika maeneo yao “Tushirikiane sana sana sisi, Wananchi viongozi wa serikali za mitaa, vijiji na madiwani kulinda miundombinu yetu ya umeme”

“Najua tumeshaongea viongozi wa serikali za mitaa vijiji na madiwani lakini niombe na Wananchi wengine wote ukiona Kuna dalili zozote zinazoweza kuharibu miundombinu wasisite kuwasiliana na uongozi wa Kijiji husika, vituo vya polisi au hata kutupigia simu tuweze kuokoa Mali ambayo ingeweza kuibiwa au kuharibiwa na tukapata hasara kubwa”

Aidha Eng. Mkaka ameshukuru Wananchi walioonyesha ushirikiano kwa kutoa taarifa mbalimbali za usalama wa miundombinu ya shirika hilo “Na nitoe wito kwa yeyote atakayeona dalili zozote ambazo sio njema atoe taarifa ili kutusaidia kuokoa miundombinu yetu kwani TANESCO ni Shirika la serikali, la umma, la Wananchi hivyo kinachoharibiwa ni cha kwetu sote”

“Tukiwajibika kulinda miundombinu yetu ambayo ni Mali yetu sote itatusaidia sisi sote kuwa na maendeleo katika mkoa wetu wa Pwani hivyo tusaidiane kwani inavyoharibiwa inaharibu Kodi za Wananchi, Mali ya umma” alisema Eng. Mkaka.

“Kwahiyo Kila mtu atusaidie kulinda au kutoa taarifa haraka ili tuweze kuzuia madhara yasitokee kwani unapotusaidia kuzuia madhara yasitokee badala ya shirika kuingia gharama za kurudishia miundombinu kwasababu inaweza kuchukua siku kadhaa kuipata na inakuwa hasara kubwa zaidi kwa serikali”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!