Home Kitaifa TUNDUMA YAPOKEA BILIONI 1,707,100,000/= TOKA MRADI WA BOOST

TUNDUMA YAPOKEA BILIONI 1,707,100,000/= TOKA MRADI WA BOOST

Na William Maganga – Tunduma TC

Halmashauri ya Mji Tunduma Imepokea pesa kiasi cha Tsh. 1,707,100,000/= kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vya madarasa, Majengo ya Utawala, Matundu ya Vyoo na Vichomea taka katika shule mbalimbali za Msingi.

Akizungumza mapema leo Afisa Elimu Msingi Bi. Casta Mbawala amesema kuwa fedha hizo zinahusisha ujenzi wa shule Mpya Mbili Moja kata ya Chapwa Mtaa wa Isanzo na kata ya Mpemba Mtaa wa Namazyanza

Aidha Bi. Mbawala amesema kuwa shule ya Msingi Fura, Mkombozi, Kigamboni, Migombani, Mlimani na Sogea zenyewe zimepatiwa pesa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na kuongeza matundu ya vyoo ili kukabiliana na wingi wa wanafunzi katika shule hizo.

Utekelezaji wa Mradi wa BOOST unatarajiwa kuboresha kiwango cha elimu na fursa za upatikanaji wa elimu kwa watoto wa elimu ya awali na msingi Tanzania Bara
Malengo mahususi ya Mradi ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu, kuinua ubora wa walimu wa shule za awali na msingi na usimamizi na utawala bora katika utoaji huduma ya elimu.

Mradi huu una afua za uboreshaji wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia kwa elimu ya awali na msingi na kwamba katika utekelezaji wake awamu ya kwanza yatajengwa madarasa Hamsini na Tano (55) ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule zilizopo ikiwa ni pamoja na kujenga shule mpya katika kata ya Chapwa na Mpemba

Afua nyingine ni pamoja kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu kufuatia utekelezaji wa mpango wa shule salama ikiwa ni pamoja na kuongeza uandikishaji kwa watoto wa elimu ya awali

Pia kuboresha uwezo na umahiri wa walimu katika ufundishaji na ujifunzaji darasani pamoja na maudhui kwa walimu, kuimarisha walimu kwa kuendeleza mafunzo ya walimu kazini, kugharimia utoaji wa elimu, kuboresha mwalimu katika matumizi ya TEHAMA kwenye ufundishaji na kuboresha mazingira ya shule

Aidha kwa fedha hizo zilizotolewa, Halashauri ya Mji Tunduma inatarajia kujenga Madarasa Mapya 55, Matundu ya vyoo 60 na Vichomea taka 02.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!