Home Kitaifa TUMUOMBEE WAZIRI ULEGA AENDELEE KUFANYA KAZI NZURI YA KUMSAIDIA RAIS DKT. SAMIA...

TUMUOMBEE WAZIRI ULEGA AENDELEE KUFANYA KAZI NZURI YA KUMSAIDIA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN – MUFTI WA TANZANIA

Na Scolastica Msewa, Mkuranga.
Mufti wa Tanzania Shehe Abubakar Zuberi bin Ally amesema anampenda Waziri wa Mifugo na uvuvi Mheshimiwa Abdallah Ulega kwa tabia yake nzuri na heshima yake kwa Mashehe na jamii amewataka Watanzania wamuombee atekeleze vyema majukumu aliyopewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Wananchi.

Amesema hayo katika ibada ya Maulidi ya mkoa wa Pwani iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya msingi Mkuranga Wilayani Mkuranga na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa dini hiyo ya kiislamu Mashehe wa mikoa mbalimbali nchini na Mombasa Kenya na Viongozi mbalimbali wa CCM na serikali.

Alisema tabia nzuri na heshima aliyonayo kwa wengine hajaiona kwa viongozi wengine wa hadhi yake “Mimi heshima kama hiyo sijawahi kuiona sijui ninyi wenzangu kama mmeshawahi kuiona kwa viongozi wengine wa hadhi yake Kweli ni Mapenzi na mahaba makubwa sana ni jambo kubwa sana tumuunge mkono tuendelee kumsaidia na tumuunge mkono.

Amesema “Ulega ni mtu wa muhimu sana anawapenda wote kwa kweli huyu tabia zake ni nzuri na ana heshima kwani hakuna kitu kizuri kama heshima kwa wengine”

“Tumuombee ili Amana aliyopewa na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan aendelee kufanya kama alivyoambiwa na kama alivyoelekezwa aweze kutusaidia na sisi katika kujenga Amani katika Taifa letu la Tanzania”

“Wakati tunakuja tulikuwa tunamzungumza garini huyu kijana Abdalah Ulega nimekutana na sampuli nyingi namjua mmoja baada ya mwingine lakini huyu ni kijana wa ajabu sana waweza ukamuita akakusubiria Waziri gani anaweza kusubiri Mbunge gani aweza kukusubiri”

“Na Shehe Nasri nae akasema huyu Waziri ni mtu mzuri hata nilipotaka kwenda kwenye gari yeye kanifungulia mpaka mlango wa gari nyie wenzangu mshawahi kuona heshima kama hiyo?”

Aidha alimtaka Waziri huyo kuwa mvumilivu na mwenye kufanya maamuzi kwa umakini ili asije kuamua vibaya.

“Ila Kila jambo utaloamua lazima ulifanyie fikra kubwa sana na ndivyo alivyo kijana wetu Abdalah mwenyezi Mungu akujalie kheri akupande na akupe Kila kitu na Kitu unachotakiwa kuwa nacho Abdalah Ulega ni kufikiri sana kabla ya maamuzi, uwe na subira uvumilivu subira ni muhimu zaidi katika kila kitu Ili usije ukaamua jambo ambalo si jema” amesema Mufti,

“Kijana wetu anatakiwa ahifadhiwe alindwe atunzwe hata Mwenyezi Mungu na kama unavyomuona ni kijana mdogo lazima agombaniwe wanamnasihi lazima tumnasihi lazima tumhofie Ili aendelee kutuangalia kututunza na kutujali”

“Juzi kwa mfano nimemuita amekuja haraka haraka halafu akakwama kwenye foleni ya magari Bado akapiga na simu shekhe nakuja nimekwamba Mbagala ila nakuja shekhe wangu na Mimi nikamwambia urudi usije maana Mimi Mbagala naijua tutaonana hata kesho inshallah akafanya hivyo na akaja haraka siku ya pili yake Mimi sijapata kuona mfano wake ndio maana nikaona kwamba ngoja tuzungumze kuwaambia watu tusije tukakosa watu wazuri”

“Wako watu fulani walikuwa na timu yao ya mpira Kisha wakamuona kocha wao ni mzembe Kisha wakamtoa bila kuwa na subira ya angalau wakae mwaka mmoja waone kama hawafungwi ama wanafungwa, ikatokea Mzee mmoja wa klabu akawashauri ,:”

“Sasa kwa sababu ya maamuzi mabaya unaweza Kuta kunafanya vibaya Kuzungumza hapa nazungumza kuhusiana na kijana wangu Abdalah Kulega usiangalie umufti ukubwa angalia watu na Mohamed alikuwaje na Mungu anasema nini”

Awali akimkaribisha Mufti katika Ibada hiyo ya Maulidi Shehe wa mkoa wa Pwani Khamisi Mtupa alisema misikiti mipya 15 inatarajiwa kujengwa katika Wilaya tano za mkoa wa Pwani ikiwemo Mkuranga, Rufiji, Kibaha, Kisarawe na Mafia.

Mtupa alisema ibada hiyo ya Maulidi imefanyika kwa ushirikiano mkubwa kati ya Mbunge wa jimbo la Hilo la Mkuranga na Waziri wa Mifugo na uvuvi Mheshimiwa Abdallah Ulega na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir Ally.

Aidha Mheshimiwa Ulega alimshukuru Mufti kwa kukubali mwaliko wa kufika katika Maulidi hiyo na alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa Waziri wa Mifugo na uvuvi kwa katika Maulidi kama hiyo mwaka jana alikuwa Naibu Waziri na sio Waziri kamili.
++++++

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!