Home Kitaifa TUME YA RAIS MABORESHO YA KODI YATUA MARA KWA KUPOKEA MAONI YA...

TUME YA RAIS MABORESHO YA KODI YATUA MARA KWA KUPOKEA MAONI YA WADAU

Na Shomari Binda-Musoma

TUME ya Rais ya maboresho ya kodi imetua mkoani Mara na kupokea maoni ya wadau wakiwemo wafanyabiashara kwa kufanya nao kikao.

Kikao hicho kilichofanyika leo januari 15 kwenye ukumbi wa Mwembeni Complex kikiongozwa na Balozi Maimuna Tarishi.

Akizungumza kwenye kikao hicho Balozi Tarishi amewataka wadau wa kodi hapa nchini kushiriki kutoa maoni na mapendekezo ili kuboresha mfumo wa kodi.

Amesema wadau wa kodi na wananchi wote kushiriki kutoa maoni kwa njia ya simu, barua Pepe, kujaza dodoso lililopo mtandaoni na tovuti ya Tume hiyo.

Balozi Tarishi amesema mapendekezo yatakayotolewa na wadau yataiwezesha serikali kuwa na mfumo mzuri wa ukusanyaji wa kodi ambao utasaidia katika maendeleo ya nchi.

” Jambo hili ni muhimu lililoanzishwa na mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na tumewafika wana Mara kwaajili ya maoni yenu.

” Tumetoa njia mbalimbali za kutoa maoni tuzitumie kufikisha maoni ili lengo la mheshimiwa Rais liweze kufanikiwa”,amesema.

Kwa upande wao wafanyabiashara na wadau mkoani Mara wameishukuru serikali kwa kuja na utaratibu wa kupokea maoni yao.

Kikao hicho kimehudhuriwa na wadau wa kodi, viongozi wa taasisi za umma na binafsi kutoka halmashauri zote za mkoa wa Mara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!