Home Kitaifa TUME YA MADINI YAKUTANA JIJINI MWANZA YAWEKA MIKAKATI

TUME YA MADINI YAKUTANA JIJINI MWANZA YAWEKA MIKAKATI

Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Profesa Idris Kikula amesema lengo la bonanza lililowakutanisha watumishi wa Tume ya madini Jijini Mwanza ni kuweka mikakati ya Tume katika suala la kukusanya mapato kutokana na miaka yote kuwa wanatumia utaratibu huo.

‘’Matokeo ni mazuri kwamba miaka yote tumefanya hapa,” Profesa Idris, Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini.

Katika hatua nyingine ya kuweka mikakati ya Tume hiyo,Timu ya mameneja wa Tume ya madini wa mikoa nchini imeifunga timu ya makao makuu ya tume hiyo magoli mawili kwa bila katika bonanza la michezo lililofanyika Jijini Mwanza katika Uwanja wa Nyamagana, linalolenga kuimarisha afya pamoja na kudumisha ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi wa tume hiyo.

Pia watumishi wa Tume ya madini wamefanya mazoezi ya viungo yaliyowashirikisha wafanyakazi wa Tume hiyo nchini pia yakiambatana na michezo mbalimbali ikiwemo riadha,mpira wa miguu,kukimbia na magunia pamoja na kukimbia na yai kwenye kijiko huku washindi wa Bonanza hilo la michezo wakipata zawadi mbalimbali ikiwemo vikombe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!