Home Afya TULINDE MAPAFU NA AFYA ZETU KWA KUJIEPUSHA NA MATUMIZI YA TUMBAKU”DK.SHANI”

TULINDE MAPAFU NA AFYA ZETU KWA KUJIEPUSHA NA MATUMIZI YA TUMBAKU”DK.SHANI”

Na Shomari Binda-Musoma

JAMII imeshauriwa kujiepusha na matumizi ya tumbaku ili kuepukana na uharibifu wa mapafu, mfumo wa upumuaji na ubongo.

Hayo yamesemwa na mganga mfawidhi wa hospital ya Wilaya ya Musoma Dk.Emanuel Shani ikiwa ni siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani.

Amesema matumizi ya tumbaku yana madhara makubwa kiafya hivyo ni vyema kujiepusha na matumizi yake kwa njia yoyote, mapafu yanapoathirika kutokana na matumizi ya tumbaku mtu hushindwa kufanya shughuli za kiuchumi na hata upelekea vifo, hivyo jamii inapaswa kuachana na matumizi yake kabisa iwe ni kwa kuvuta au kutafuna kutokana na madhara yake.

Yapo madhara mengi ya matumizi ya tumbaku ya moja kwa moja na zipo kemikali ambazo uathiri mwili kwa mtumiaji, Licha ya kuathiri mapafu na mfumo wa upumuaji pia unaathirika hivyo ninaishauri jamii iachane kabisa na matumizi ya tumbaku “,amesema.

Dk.Shani amesema kwa sasa umeibuka ulevi wa uvutaji wa shisha unaochanganywa na tumbaku kwenye kumbi za starehe jambo ambalo ni hatari kwa afya.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na Mzawa Blog wamesema licha ya tumbaku kuwa zao la kibiashsra inapaswa kuwekwa sheria kutokana na matumizi yake, wapo watu wanaovuta ovyo tumbaku na kuwasababishia madhara wengine kama vile ugonjwa wa moyo, shinikozo la damu, saratani ya tumbo, mfumo wa uzazi na kiarusi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!