Home Kitaifa TUHUMA MBALIMBALI KUHUSU MAMLAKA YA HIFADHI YA ENEO LA NGORONGORO

TUHUMA MBALIMBALI KUHUSU MAMLAKA YA HIFADHI YA ENEO LA NGORONGORO

Wizara ya Maliasili na Utalii inazo taarifa za madai na tuhuma mbalimbali zinazowahusu Watumishi kadhaa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro ambazo zimekuwa zikisambazwa na Mitandao ya Kijamii na Vyombo vya Habari.

Taarifa hiyo  imetolewa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini John Mapepele  aprili 02, 2024 Dodoma

Wizara inauhakikishia umma kwamba tayari ilishaanza kuzifanyia kazi kwa kushirikisha vyombo mbalimbali vya Serikali kabla ya mitandao ya Kijamii kuanza kuzisambaza. “Serikali itachukua hatua kali za kisheria dhidi ya Watumishi watakaobainika kuhusika.

Aidha, Wizara inautaarifu umma kwamba hakuna mabadiliko yoyote katika Zoezi la Uhamaji wa Hiari kutoka Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na hali kadhalika shughuli za uhifadhi na utalii zinaendelea kama kawaida.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!