Home Burudani TUFUGE MIFUGO KISASA TUENDELEE KUPATA NYAMA YENYE UBORA SOKONI” RC MTAMBI”

TUFUGE MIFUGO KISASA TUENDELEE KUPATA NYAMA YENYE UBORA SOKONI” RC MTAMBI”

Na Shomari Binda- Butiama

MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Enock Mtambi amewataka wafugaji mkoani humo kuendelea kufuga kisasa ili kupata soko zuri sokoni.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mwalimu Moses Kaegele akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo leo juni 6 kwenye tukio la kwanza la mashindano ya nyama choma yaliyofanyika mnada wa Kiabakari.

Amesema ufugaji wa kisasa ndio utapata nyama bora, mkoa wa Mara ni mkoa ambao unaongoza kwa kuwa na mifugo mingi na lazima itumike kuongeza uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.

Mkuu huyo wa Wilaya kwa niaba ya mkuu wa mkoa amesema kuwa na mifugo mingi haitoshi bali ni kuwa na mifugo iliyofugwa kisasa ili kupata masoko, ng’ombe,mbuzi,kondoo zilizopo mkoani Mara mifugo hiyo itumike kuongeza uchumi wa mkoa na wananchi wake.

Nipo hapa kwa niaba ya mkuu wa mkoa ambaye ndiye aliyeanzisha mashindano haya ambayo yanazinduliwa leo na yatakuwa endelevu.

Mkuu wa mkoa anataka mifugo iendelee kufugwa kisasa bila kupigwa sana na kupoteza ladha ya nyama ili kuendelea kufanya vizuri kwenye masoko“,amesema.

Amesema tukio la nyama choma ni fursa pia kwa wachomaji nyama kuwatangaza ili washindi na washiriki waweze kufahamika na kushiriki matukio mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Mara.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Butiama Marwa Siagi amempongeza mkuu wa mkoa wa Mara kwa kuja na wazo hilo ambalo limeijenga wilaya ya Butiama na mkoa wa Mara.

Amesema tuko hilo sio dogo na limepata muitikio mkubwa japo ni kwa mara ya kwanza na limetangazwa kwa muda mfupi.

Jumla ya washiriki 32 wa kuchoma nyama ambapo washindi wamepewa zawadi huku mashindano hayo yakitangazwa kuwa endelevu

Mshindi wa kwanza wamekuwa Rwamkoma JKT waliopata zawadi ya shilingi laki 5,Deus John amekuwa mshindi wa pili na kupata zawadi ya shilingi laki 3 na Ramaa hotel wamekuwa washindi wa 3 na kupata shilingi laki 1 na nusu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!