Home Kitaifa TUCTA PWANI YALILIA BOTI KWA AJILI YA USAFIRI WA WALIMU WANAOFUNDISHA KATIKA...

TUCTA PWANI YALILIA BOTI KWA AJILI YA USAFIRI WA WALIMU WANAOFUNDISHA KATIKA SHULE ZILIZO KWENYE MAENEO YENYE MAFURIKO YA MTO RUFIJI HUKO DELTA KIBITI

NA Scolastica Msewa, Kibiti.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni Mfanyakazi Bora mchapakazi wa kwanza katika mkoa wa Pwani kwa kuboresha maslahi na kuboresha miundombinu ya Wafanyakazi wa mkoa huo.

Amesema hayo wakati akihutubia Katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi duniani kimkoa yaliyofanyika katika Wilaya ya Kibiti Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema Rais Dkt. Samia anawapenda na kuwathamini sana Wafanyakazi wa mkoa wa Pwani na ukweli Wafanyakazi wanauona.

Mheshimiwa Rais anaangaika sana kuangalia namna gani anaongeza uwezo wa serikali kuboresha mazingira ya kazi nchini ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya shule ambazo watoto wanasoma, sekta ya afya na tayari ameahidi kuboresha makazi ya Wafanyakazi katika sekta ya elimu na afya.

“Walimu mpate nyumba, Watu wa afya mpate nyumba na sehemu zingine tumeshaanza lakini wanasema unashona koti kulingana na ukubwa wa kitambaa ulichonacho huwezi kufanya mambo kama uwezo bado ni mdogo.” Alisema Kunenge.

Alisema serikali inafahamu kazi kubwa inayofanywa na Wafanyakazi wa sekta, idara na Taasisi mbalimbali katika kuhudumia Wananchi na kumsaidia kazi Rais mkoani humo.

Hatahivyo Kunenge aliwataka Wafanyakazi mkoa wa Pwani kufanya kazi kwa bidii ilikuongeza tija katika utendaji kazi wao kwa Wananchi ili kuboresha maisha ya Wananchi mkoani Pwani.

Aidha aliwataka kuzungumzia kazi nzuri anazofanya Rais Dkt Samia katika kuhudumia Wananchi nchini “mnapopata nafasi semeni mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye anawapenda na kuwajali Wafanyakazi nchini kwani anawahakikishia usalama, haki za Wafanyakazi kazini”

Akizungumzia changamoto mbalimbali walizoziwasilisha kupitia risala ya Wafanyakazi Mkuu huyo wa mkoa wa Pwani alisema Kuna masuala mengi tayari serikali imekwishaanza kuyashughulikia ikiwa ni pamoja na suala la kikokotoo cha wastaafu.

Awali Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania TUCTA mkoa wa Pwani Kinyogoli Ramadhani ameomba serikali kuangalia namna ya kusaidia usafiri wa uhakika kwa Walimu wanaofundisha katika Shule za maeneo ya Kata za Delta ambako kutoka sehemu Moja kwenda nyingine hutumia mitumbwi.

Hatahivyo katika maadhimisho hayo kumefnyika harambee ya kuchangia fedha na misaada mbalimbali kwaajili ya Waathirika wa mafuriko ya Mto Rufiji na Kibiti ambapo shilingi zaidi ya milioni 4,400,000/- zilipatikana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!