Home Kimataifa TUCHANGAMKIE FURSA ZIPATIKANAZO KUPITIA DIPLOMASIA YA UCHUMI-BALOZI, PROF. KILANGI.

TUCHANGAMKIE FURSA ZIPATIKANAZO KUPITIA DIPLOMASIA YA UCHUMI-BALOZI, PROF. KILANGI.

Balozi wa Tanzania Nchini Blazili Mhe.Prof Adelardus Kilangi, amewataka Watanzania kuchangamkia fursa zinazopatikana kupitia Diplomasia ya uchumi katika ujumla wake.

Akizungumza na wanahabari kwa njia ya mtandao kupitia ‘Tanzania Watch’ Mhe,Balozi amesema fursa hizo zinapatikana kupitia uwakilishi wa Tanzania katika nchi mbalimbali kupitia balozi zetu.

“Malengo ya mkutano huu ni kuainisha fursa zinazopatikana na namna ubalozi wa Tanzania Nchi Blazili ulivyojipanga kuwasaidia watanzania kuchangamkia fursa hizo” amesema Prof.Kilangi.

Akielezea maana ya diplomasia ya uchumi Mhe.Balozi amesema ni kutumia michakato na duru za kidiplomasia ili kuvutia kukua kwa uchumi na kupata maendeleo kwa ujumla hasa kiuchumi na kijamii, hivyo kuvutia uwekezaji,kuvutia biashara kuuza na kununua nje ya Tanzania, na kuwezesha kuhaulisha teknolojia,ujuzi,utaalamu maarifa na kuwezesha kuboreshwa kwa huduma za kijamii.

Akielezea wajibu wa Balozi za Tanzania nje ya nchi Mhe.kilangi amesema kazi kuu ni Diplomasia ambayo ndani yake Kuna Diplomasia ya uchumi,lakini mkuu wa Nchi (Rais) ndiye mdiplomasia namba moja akifuatiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na ndio anafuata Balozi na ubalozi kwa ujumla.

“Ubalozi na Balozi kwa ujumla ni mwakilishi wa mkuu wa Nchi, mwakilishi wa Nchi na Serikali na katika jukumu la diplomasia ya uchumi,ubalozi unafanya kazi ya kutafuta fursa na kuzibainisha” aliongeza Balozi Kilangi.

Kwa upande wa wanufaika wa fursa hiyo ya diplomasia ya uchumi Mhe.Balozi amesema walengwa wakubwa ni Serikali,Sekta ya Umma, Sekta Binafsi,Sekta isiyo ya Kiserikali wakiwemo pia Wafanyabiashara,wenye Viwanda,Wakulima,Taasisi za Elimu, Afya na wote wanaojihusisha na Shughuli za kiuchumi.

Akizungumzia namna ubalozi wa Tanzania Nchi Blazili unavyowatafutia fursa watanzania Prof.Kilangi amesema wameshafanya mawasiliano na Jumuiya ya wenye viwanda Tanzania kupitia Mamlaka husika ili kuanzisha mahusiano na kuwawezesha wadau husika kupata mafunzo nchini Brazili ambapo hawatatozwa gharama yoyote,isipokuwa gharama za kuishi peke yake.

Kwa upande wa michezo Mhe.Balozi amesema tayari wamefanya ziara ya kikazi ya ubalozi mjini Sao Paulo na waliweza kutembelea na kufanya mazungumzo na mkurugenzi wa kituo cha kuendeleza Mpira wa Miguu cha Zicco.

“Ubalozi uliweza kushawishi kituo cha Zicco na kukubali kushirikiana na Tanzania katika kufundishia timu ya mpira wa miguu ya vijana chini ya miaka 17 na 15 na kuwajengea uwezo makocha wa timu hizo” amesema Balozi Kilangi.

Aidha ameongeza kuwa pia kituo hicho kilikubali kuipokea timu ya Taifa ya vijana kwenda kufanya mazoezi Brazili pamoja na kucheza mechi za kirafiki kwa lengo la kuendeleza vipaji vya soka kwa vijana wa kitanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!