Na Magrethy Katengu
BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imesema Mwaka huu Vivutio vya Utalii na wadau wa huduma za Utalii nchini wameibuka washindi katika mashindano yaliyotangazwa katika hoteli ya “Atlantis the Royal” Dubai Oktoba 15, 2023.
Hayo yamebainishwa jana Oktoba 17 2023 na Mkurugenzi wa Masoko wa TTB Dkt. Glastone Mlay akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) inawajulisha Umma kuwa mtandao wa WORLDT RAVEL AWARDS mwaka huu 2023 umetangaza washindi mbalimbali kwenye Mashindano yanayohusisha, Vivutio vya Tanzania, Bodi za nchi zinazosimamia Utalii, Makampuni yanayojishughulisha na Utalii Afrika na Duniani kote katika nyanja mbalimbali,” amesema Dkt. Mlay na kuongeza,
“Mwaka 2023, TTB na Taasisi za wizara zilishirikiana na sekta binafsi kwenye kutangaza vivutio na hatimaye kupigiwa kura kwa ubora na vigezo vilivyowekwa na World Travel Awards kuanzia tarehe 17 Novemba,2022 hadi tarehe 22 Mei 2023,”.
Hivyo amebainisha kuwa baada ya kupigiwa kura na ukaguzi wa huduma duniani, Mtandao wa World Travel Awards 2023 umetoa tuzo za Ushindi kwa mchanganuo ufuatao;-
Mosi, kushindanishwa kwa Bodi za Utalii Barani Afrika (Africa’s leading Tourist Board) kwamba Bodi za nchi 12 za Botswana, Misri, Gambia, Ghana, Kenya, Morocco, Namibia, Nigeria, Rwanda, Afrika Kusini, na Zambia zilishindanishwa na iliyoibuka mshindi wa kwanza ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Pili, kampuni inayoongoza Watalii (Africa’s leading Tour Operators) hapa makampuni mbalimbali 13 yalishindanishwa barani Afrika na iliyoibuka mshindi ni ZARA Tours ya Tanzania.
Tati, katika kundi la Eneo la uhifadhi lenye kuvutia Zaidi katika Afrika (Africa’s Leading Tourist attraction) hapa kwenye kundi hili eneo la Ngorongoro (NCA) limeibuka Mshindi.
Nne, kundi la Hifadhi za Taifa Afrika (Africa’s Leading National Park) Hifadhi ya Serengeti imeongoza.
Tano, Sehemu za mapumziko (Africa’s Leading new Resorts) kwenye kundi hili mshindi barani Afrika ni Emerald Zanzibar Resort & Spa.
Sita, kundi jingine ni la tenti za starehe zenye hadhi ya juu (Africa’s leading Luxury tented Safari camp) iliyoshinda barani Afrika ni Siringit-Serengeti Camp Tanzania.
Saba, katika kundi la visiwa vipya venye hadhi ya juu kwa kuvutia watalii barani Afrika (Africa’s new leading Luxury Islands) ni kisiwa cha Thanda kilichoko katika wilaya ya Mafia Tanzania ndicho kimeongoza.
Nane, pia kampuni mbalimbali ziliingia kwenye ushindi wa aina mbali mbali ndani ya nchi na zilizoongoza ni kampuni ya ndege ya Auric, na nyingine ni kama vile, “First Rental Tanzania”, Zanzibar Serena Hotel, Gran Melia Arusha, Melia Zanzibar, Twiga Tours, Lamai Serengeti, Kuro Tarangire. Makampuni mengine ni Green Inspirations DMC, Zara Tours, Satguru Travel Tanzania, FCM travel-Tanzania Skylink Travel & Tours na mengineyo.
Dkt. Mlay ameeleza kuwa ushindi huu unaendelea kuiweka Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye ramani ya Dunia na kuongeza idadi kubwa ya watalii.
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) inawashukuru sana, World Travel Awards na wadau wote walioshiriki katika mchakato mzima aliosababisha ushindi huo bila kuwasahau waliopiga kura na kuwezesha vivutio,