Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeendela kusisitiza kwamba halina mgogoro wa kimalipo na kampuni ya Eurowagon ya nchini Uturuki ambayo ilipewa zabuni ya kutengeneza mabehewa 30 na vichwa 2 vya treni ya umeme.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa kitengo cha habari na uhusiao Jamila Mbarouk amesema kwamba TRC ilitimiza matakwa ya mkataba ya kulipa 35% na kwakutimiza masharti ya umiliki wa vichwa vya treni ya umeme ilihamia kwa TRC.
Aidha ameendelea kusema kwamba mkataba unatoa haki kwa TRC kuchukua majukumu ya kumalizia ukarabati mara pale mzabuni anaposhindwa kutimiza masharti ya mkataba hata hivyo mkuu huyo wa mahusiano wa TRC hakubainisha masharti ambayo kampuni iliyopewa zabuni kushindwa kutekeleza masharti ya mkataba.
“Katika kuhakikisha uendeshaji wa awali unaanza baada ya majaribiao mara baada ya ujenzi kukamilika TRC ilisaini mkataba wa vifaa vichache wa muda mfupi wa ununuzi wa vichwa vya treni ya umeme viwili na behewa 30 za abiria vitakavyo fanyiwa ukarabati kutoka kampuni ya Eurowagon ya nchini Uturuki”amesema Jamila.
Nakuongeza kwamba kwa mujibu wa mkataba vifaa vilitakiwa kukamilika mnamo mwezi Novemba 2021 kwakuwa kampuni ya Eurowagon ilishindwa kutimiza matakwa ya kimkataba na kipande cha kwanza Dar es salaam hadi Morogoro,kipo hatua ya mwisho ya ujenzi,TRC iliamua kusitisha mkataba na kuwajulisha kwa barua mnamo tarehe 25 februari 2022, TRC iliendelea na jukumu la kumaliza ukarabati bila gharama na vifaa vinatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi wa 8,2022.
Hatua hiyo imekuja baada ya chombo kimoja cha habari hapa nchini kulipoti kuwa TRC inamgogoro na Kampuni ya Eurowagon nakusema kwamba TRC imepokea mabehewa na vichwa vya treni vilivyotumika (mtumba).
Show quoted text