Home Kitaifa TRC BORESHENI HUDUMA HUSUSANI KWA WASAFIRISHAJI WA MIZIGO

TRC BORESHENI HUDUMA HUSUSANI KWA WASAFIRISHAJI WA MIZIGO

Na Magrethy Katengu

WAZIRI wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa ameitaka Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhakikisha inaisimamia Menejimenti kwenye eneo la uendeshaji na kuboresha utoaji wa huduma hususani kwa wasafirishaji wa mizigo.

Amebainisha Jijini Dar es Salaam wakati akizindua bodi mpya ya shirika la Reli ambapo u amesema utoaji huduma kwa ufanisi katika reli utaongeza mzigo na kulifanya shirika hilo kuweza kujiendesha kwa faida badala kutegemea fedha za serikali

“Kwenye eneo la ujenzi mnakwenda vizuri lakini bado kwenye uendeshaji hakuna utendaji mzuri, leo wasafirishaji wana mzigo wa kutosha lakini wakija kutafuta mabehewa wanaambiwa wakae foleni, hii haiwezekani kuendelea namna hii mmekuwa mkilalamikiwa ucheleweshaji wa utoaji wenu huduma hauridhishi Mwenyekiti simamia hili’ amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa ameeleza umuhimu wa matumizi ya tiketi mtandao kwa abiria na kuitaka TRC kuboresha mifumo ili kupunguza usumbufu unaojitokeza kwa abiria wanaolazimika kukaa muda mrefu kusubiria kukata tiketi wanapotaka kusafiri Dunia inakwenda Kasi na teknolojia bado mko kizamani utoji tiketi badilikeni.

Aidha, Prof. Mbarawa ameongeza kuwa seriki ina lengo la kuhakikisha reli zote mbili zinakuwa na tija hivyo ameitaka TRC kuchukua hatua stahiki kwa kutafuta wabia watakaoendesha treni mara baada ya ujenzi na ukarabati kukamilika.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara amesema Serikali itaendelea kuhakikisha fedha inazotenga kwenye bajeti za kila mwaka zinatumika katika kuboresha shirika hilo ambalo bado linahitaji vitendea kazi ili kujiendesha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Ally Amani amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa Bodi imejipanga kutumia uzoefu ulionao kuhakikisha shirika hilo linakuwa na tija na kujiendesha kwa faida siyo kihasara na watafanyia kazi maelekezo yote waliyopewa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!