Na Mariam Muhando_ Dar es salaam.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania TRA imeahidi kushirikiana na Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania JUMIKITA ili kufanikisha mipango ya Maendeleo kupitia ukusanyaji Kodi.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano wa TRA Hudson Kamoga katika semina iliowakitanisha JUMIKITA na TRA Jijini Dar es salaam Kwa lengo la kupata elimu ya Mlipakodi.
Kamoga amesema lengo la ushirikiano huo ni kuimarisha ushirikiano na Jamii kupitia waandishi hao ambapo TRA wakiitumia jumuia JUMIKITA itakuwa rahisi elimu ya Mlipakodi kuwafikia watu wengi kwa haraka kwenye njia ya Mitandao.
“Tumetumia fursa hii katika kuwapa elimu ya masuala mbalimbali nayohusu TRA ikiwemo makusanyo ya Kodi ya Kidigitali, umuhimu ya kudai risti unapofanya manunuzi, mambo ya forodha, EFD, ETS na huduma kwa mteja“, amesema Kamoga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa JUMIKITA Shabani Matwebe ameipongeza TRA kwa kuwa Taasisi ya kwanza ya Serikali kutambua na kuthamini nguvu ya mitandao ya kijamii.
“TRA ni Taasisi ya kwanza kugundua nguvu ya Digital Platform, Nyie mnajua ni jinsi gani mnapata tabu kupata taarifa ikitokea mtu amewatambua ni lazima tumpongeze, Digitali Platform haikwepeki, Mkurugenzi nikupongeze,” amesema Matwebe.