Home Kitaifa TPDC KUJENGA MIUNDOMBINU YA KUCHAKATA GESI NA KUISAFIRISHA MPAKA DAR ES SALAAM

TPDC KUJENGA MIUNDOMBINU YA KUCHAKATA GESI NA KUISAFIRISHA MPAKA DAR ES SALAAM

Na Magrethy Katengu

Serikali kupitia shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania TPDC imeweza kujenga miundombinu ya kuchakata gesi na kusafirisha gesi asilia kutoka Madimba Mtwara na Songosongo (Lindi) hadi Dar es salaam yenye thamani ya takribani trillion 2

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam na Jukwaa la Wahariri TEFF pamoja na waandishi wa habari katika semina elekezi MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC), Mussa Mohamed Makame amesema shirika linaendelea kuweka michakato kusaidia upatikanaji wa gesi kila mahali ikiwemo kutengeneza kituo mama cha gesi Dar es Salaam, ili kurahisisha upatikanaji wa gesi nchi nzima.

Mkurugenzi Makame amesema shirika hilo limedhamiria kutoa huduma ya gesi nyumbani na kwenye magari, hivyo ni lazima wawe na vituo vingi kwa ajili ya kuhakikisha bishara hiyo ya gesi inafanyika na wananchi wanapata nishati inapatikana kwa uhakika

Mradi tunaotekeleza sasa ni kujenga kituo mama cha usambazaji wa gesi iliyoshindiliwa, tunajenga maeneo ya Mlimani City Dar es Salaam, kituo hicho kitakuwa kinashindilia gesi ili itiwe kwenye malori ambayo yatakuwa yakisambaza gesi katika vituo dada vitakavyojengwa,ikiwemo Mwenge-Mbezi Beach lakini pia kitakuwa kinajaza magari palepale,” amesema Makame

Mkurugenzi huyo amesema wametoa pia fursa kwa Wawekezaji kampuni binafsi kujenga vituo vitakavyotoa huduma ya gesi ya majumbani , ili kufikia lengo la kusambaza huduma hiyo maeneo mbalimbali nchi nzima

Kwa upande wake Mkurugenzi wa utafutaji na uendelezaji gesi asilia, Keneth Mutaonga amesema shirika hilo lipo katika hatua za mwisho kuelekea kuanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa gesi ambao utaongeza gesi , pato la taifa na kutengeza ajira.

Hata hivyo amesema kuwa Shirika limekuwa likizingatia ushiriki wa wazawa kwenye masuala. ya mafuta na. gesi na miradi ya kisekta inayoyekelezwa. hapa nchini kwa kupata fursa za ajira ikiwemo ukandarasi , ulinzi hivyo watanzania wasilalamike wachangamkie fursa zinazojitokeza katika miradi hiyo

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile amesema Watanzania wasiwe watu wa kulalamika lalamika kusikokuwa na faida mindong’ono mingi wanapoona Kuna uwekezaji unafanyika watambue kuwa hakuna nchi inayoendelea pasipokuwa na uwekezaji na kukopa fedha ili watekeleze miradi yao ya kimkakati

Aidha Miradi hiyo ina faida kubwa kwa taifa na kuwataka waandishi wa habari kuisemea miradi hiyo pamoja na kutoa uelewa kwa wananchi, ili kuondoa baadhi ya upotoshaji ambao umekuwa ukisambazwa kwenye jamii juu ya masuala mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!