Home Kitaifa TPA TANGA YAIBUKA KINARA WA TUZO MAONYESHO YA BIASHARA 2023

TPA TANGA YAIBUKA KINARA WA TUZO MAONYESHO YA BIASHARA 2023

Na Boniface Gideon, TANGA

MAMLAKA ya Usimamizi wa bandari (TPA’)Tanga imeibuka kuwa mshindi wa jumla katika maonyesho ya biashara na utalii yaliyofanyika katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga kwa mwaka 2023 yaliyoandaliwa na chemba ya biashara.

Maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka mkoani Tanga yakihusisha taasisi, kampuni na mashirika ya kiserikali na yasiyokuwa ya kiserikali kwa lengo la kutoa huduma kwa wananchi sambamba na wafanyabiashara mbalimbali wakitangaza biashara zao.

Akizungumza mara baada ya kuhitimishwa rasmi na mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba June 6,2023 kaimu meneja wa mamlaka ya Bandari Tanga Petter Milanzi alisema kuwa wamekuja kivingine katika utoaji wa huduma bora kwa wadau na wafanya biashara wote wa ndani na nje ya nchi wanapotumia bandari hiyo.

Tanga sasa ni lango kuu la uchumi wa afrika mashariki na sisi tunasema bandari ni lango la biashara kitaifa na kimataifa na tumekuja katika maonyesho ya biashara na utalii kuwahakikishia wateja wetu kwamba wafike na waitumie bandari yetu ya Tanga na sisi tutawapa huduma bora ambazo wanazitarajia katika viwango vya kimataifa”

Sasa hivi bandari ya Tanga imezaliwa upya maana yake sisi sasa mambo mengi tunayafanya kimataifa na ndio maana tumekuwa washiriki wa kwanza katika vipengele vyote vilivyoshindanishwa katika maonyesho ya biashara na utalii kwa mwaka 2023 na tulikuwa wafadhili wakubwa ili kuhakikisha maonyesho haya yanafanyika kwa ufanisi zaidi” alisema Milanzi.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha masoko katika bandari hiyo Rose Tandiko ambao pia ndio wadhamini wakuu wa maonyesho hayo tangu yalipoanzishwa mwaka 2013 alisema kuwa wameyatumia vyema kwa kuwapa elimu washiriki na wadau mbalimbali waliojitokeza ambapo wameongeza wigo mpana kwa watumiaji wa bandari hiyo.

Bandari ya Tanga sasa imekuwa mpya vifaa vimeongezwa vimekuwa vingi ari ya utendaji kwa wafanyakazi wa bandari ya Tanga imeongezeka kwa kiwango cha juu zaidi na wako tayari kuhudumia meli za aina yoyote na mizigo yeyote kwa sababu vifaa vipo tumewezeshwa na serikali” alisema Tandiko

Ukiacha kutoa elimu kwa wale ambao hawafahamu kazi zetu tumeweza kukutana na wadau wengi ambao tunafanya nao kazi kupitia bandari tuweza kupata mrejesho wa huduma zetu kutoka kwao na sisi tumepokea maoni yao kwaajili kwenda kuboresha utendaji kazi wetu” alisema Tandiko.

Bandari ya Tanga ambayo imefanyiwa maboresho makubwa kwa upanuzi wa kina cha bahari na ukarabatI wa gati mbili kupitia fedha zilizo wekezwa na serikali zaidi ya billion 400 na kuwezesha meli kubwa kutoka nchi mbalimbali kushusha mizigo na kupakia bandarini hapo tofauti na miaka ya nyuma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!