Home Burudani TOSHCARGO NA TPBRC YAJA NA KUBWA KULIKO, TUZO MBALIMBALI KUSHINDANIWA

TOSHCARGO NA TPBRC YAJA NA KUBWA KULIKO, TUZO MBALIMBALI KUSHINDANIWA

Na Magrethy Katengu

Kampuni ya usafiriji mizigo leo imezindua tuzo za mwaka 2023/2024 kwa ngumi za kulipwa katika vipengele mbalimbali ikiwemo bondia bora wa mwaka wa kike na kiume pamoja na wakala bora wa mwaka muamuzi bora wa mwaka ili kusaidia kutoa hamasa kwa wadau wa ngumi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam Mkurigenzi wa Masoko Toshcargo Amitin Abubakar amesema wameingia kudhamini tuzo hizo hizo ni kusaidia wanaoingia katika mapambano ili vijana na wapenzi wa mchezo huo waupende na kusaidia kuibua vipaji vya vijana wa ambao walikata tamaa .

Amitin amebainisha kuwa mchakato huo utaanza mwezi Marchi 2024 kwa watu kupiga kura kuchagua vipengele vinavyoshindaniwa huku ukihitimishwa kwa kutoa tuzo June 2024 .

Kwa upande wake, Katibu Kamisheni wa ngumi za kulipwa TPBRC, George Lukindo ameshukuru sana Tosh Cargo kuwa wadhamini kwani tuzo hizo ni kwa mara ya kwanza kutolewa kwa mchezo huo na zitakuwa zikitolewa ki mwaka na inakwemda kuhamasisha mabondia kupenda mchezo huo.

Tuzo hizi zipo katika vipengele ikiwemo bondia bora wa kiume wa mwaka na wakike, muandaaji bora, muamuzi bora,wakala bora, kocha bora, muandishi bora wa habari, chombo bora, bondia bora chipukizi, msherehashaji bora,meneja bora, kocha bora, pambano bora, nokaunt bora.

Naye Bondia Leila Macho amemuomba Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwaunga mkono mabondia kwa kutoa hamasa kama anavyotoa hamasa goli moja milion tano katika mpira wa miguu .

Na sisi tunakumbana na changamoto za kufanya mazoezi katika mazingira magumu vipato vyetu ni vidogo hivyo wengine wamekata tamaa kucheza mchezo huhu hivyo serikali ituangalie kwa jicho la tatu kwani bodo hali yetu siyo nzuri kufanya vizuri katika mapambano.

Naye Dulla Mbabe ameshukuru sana kampuni hiyo kuingia kudhamini tuzo hizo kwa mara ya kwanza kwani wamekuwa wakiishia kushuhudia wanamziki wasanii wakipewa tunzo za heshima hivyo watahakikisha wanafanya vizuri kataifa na kimataifa kupeperusha bendera ya Tanzania kupitia mchezo huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!