Home Kitaifa TMDA YATAJA KEMIKALI SUMU ZAIDI YA 90 KATIKA BIDHAA ZA TUMBAKU

TMDA YATAJA KEMIKALI SUMU ZAIDI YA 90 KATIKA BIDHAA ZA TUMBAKU

Na Andrew Chale, Dar es Salaam,
 
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba [TMDA], imebainisha kuwa, bidhaa za tumbaku zina Kemikali sumu mbalimbali ikiwemo zinazosababisha Magonjwa ya Kansa huku wakibainisha Kemikali zaidi ya 90.

Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo, kwenye maonesho ya Kimataifa ya wadau wa bidhaa za afya ya Afrika Mashariki yanayofahamika ‘Pharmatech East Afrika’ yaliyoanza Agosti 30, 2022 ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Bw. Fimbo amesema kwa sasa Serikali imewekeza mashine za kisasa za kupimia Kemikali sumu katika bidhaa zote za tumbaku ikiwemo Sigara,

“TMDA tupo hapa tunashiriki kutoa elimu kama wadau sekta ya madawa na vifaa tiba.

Ambapo pia mgeni rasmi, Mhe Naibu Waziri, wa Wizara ya Afya, Dkt. Godwin Mollel alipata wasaha wa kutembelea banda letu kupata maelezo juu ya Kemikali sumu za kwenye tumbaku.”Alisema Adam Fimbo.

Na kuongeza kuwa:
“Kemikali sumu hizi zinasababisha kansa ya damu, kansa ya koo, na magonjwa mengine yasiyo ya kuambukiza,

Zikikosekana hizi kwenye bidhaa za tumbaku ndio inapunguza magonjwa kama ya kansa, kubwa zaidi tunataka tuwaoneshe wadau mbalimbali wanaofika kushiriki kwenye maonesho haya,” Alisema Adam Fimbo.

Pia amesema bidhaa zozote za tumbaku ikiwemo Sigara zinazoingizwa nchini wanazipitia na endapo wakiona zina Kemikali sumu hizo wanaziondoa sokoni.

Baadhi ya Kemikali sumu hizo ambazo TMDA wameziorodhesha ni pamoja:

Acetaldehyde, Acetamide, Acetone, Acrolein, Acetamide, Anabasine, Arsenic, Anisidine, O-anisidine, Ammonia, Catechol, Carbon monoxide, Caffeic acid, Cobalt, Furan, Hydrogen cyanide, Lead, Mercury

Lakini pia zipo Kemikali sumu za : Nicotine, Nickel, Nitromethane, Ndela, Selenium, Quinoline, Styrene, Uranium 235 na uranium 238 na zingine nyingi.

Aidha, Adam Fimbo amebainisha kuwa, dawa ambazo hazijasajiliwa hazipaswi kuwepo nchini ambapo kwa watakaohusika na dawa hizo watachukuliwa hatua za kisheria zilizopo.
 
Ambapo amesema kuwa, dawa duni zipo kwa asilimia ndogo na wanaendelea kutoa elimu kwa njia mbalimbali ilikuwafikia Wananchi na Wadau ukiwemo kushiriki maonyesho hayo.
 
Maonesho hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika kwa siku tatu katika ukumbi huo wa Diamond Jubilee jijini Dar Es Salaam, yatafikia tamati, Septemba Mosi, mwaka huu

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!