Na Magrethy Katengu
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mwelekeo wa mvua za masika kwa mwezi Machi hadi Mei 2023 itakuwa jumla za Mvua za Wastani zinatariwa kunyesha katika maeneo mengi ikiwemo Mikoa ya Kagera,Kagera, Mwanza Arusha,Kilimanjaro ,Shinyanga.
Akizungumza na waandisha wa habari leo Februari 22, 2023 jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Ladislaus Chang’a amesema kutokana na Mifumo ya hali ya hewa inayotarajiwa katika kipindi Cha msimu na mvua za wastani Hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ikiwemo Mikoa ya Dar es salaam (Pwani) visiwa vya Mafia Kaskazini Morogoro na Kisiwa cha Unguja.
“Mvua za msimu zilizoanza Mwezi Novemba 2022 Hadi Januari 2023 mvua hizi zilitawaliwa na vipindi virefu vya ukavu hususani Mwezi Novemba 2022 kwa maeneo ya Pwani ya kusini Mkoa wa Morogoro na katika kipindi kilichosalia cha msimu Februari,Machi na Aprili mvua zinatariwa kunyesha kama ilivyotabiriwa mwezi Octoba 2022″amesema Kaimu Mkurugenzi
Dkt. Chang’a amefafanua kuwa Mvua za masika zinatarajiwa kuwa Wastani hadi chini ya Wastani katika maeneo mengi ya ukanda wa ziwa Victoria pamoja na Kaskazini Mkoa wa Kigoma na Mvua hizo zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Machi ,2023 na kuisha wiki ya nne ya mwezi Mei,2023.
Akitoa maelezo ya kina juu ya mwelekeo wa mvua hizo za msimu kwa Kanda ya Ziwa Victoria inayojumuisha mikoa ya Kagera, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara) pamoja na Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma (wilaya za Kakonko na Kibondo).
Kwa ukanda wa Pwani ya Kaskazini yaani Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Mkoa wa Pwani (ikijumuisha kisiwa cha Mafia), Dar es Salaa, Tanga pamoja visiwa vya Unguja na Pemba):
Dkt. Chang’a amesema Mvua za Wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (ikiwemo visiwa vya Mafia), Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro na kisiwa cha Unguja.
“Aidha, Mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa kunyesha katika maeneo ya mkoa wa Tanga pamoja na kisiwa cha Pemba. Mvua hizo zinatarajiwa kuanza wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Machi, 2023 na kuisha Juni, 2023,” ameeleza Dkt. Chang’a.
Kwa Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro) amesema Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani na zinatarajiwa kuanza wiki ya pili na ya tatu ya mwezi mwezi Machi , 2023 na Mvua hizo zinatarajiwa kuisha wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Mei, 2023.
Msimu wa mvua za Masika ni mahususi kwa maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki, (mikoa ya Arusha, Manyara, na Kilimanjaro), Pwani ya Kaskazini (kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, mikoa ya Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Dar es Salaam, Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba), ukanda wa Ziwa Victoria (mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara) pamoja na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma.
Aidha TMA imetoa angalizo Kwa kusema mwelekeo wa mvua uliotolewa umezingatia zaidi kipindi cha msimu wa miezi mitatu na hali ya mvua katika maeneo makubwa hivyo viashiria vinachangia mwenendo wa mfumo wa mvua na mabadiliko ya muda mfupi katika maeneo madogo utazingatiwa katika uchambuzi wa utabiri wa muda wa kati na mfupi hivyo Watumiaji wa taarifa za utabiri wa saa 24 ,siku 10,mwezi na tahadhari kama zinavyotolewa.