Na Magrethy Katengu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Kijazi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwelekeo wa msimu wa mvua za Oktoba hadi Desemba mwaka huu (vuli) Jijini Dar es Salaam.
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza msimu wa mvua za vuli unatarajiwa kuwa na mvua za chini ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi ya nchi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi kuhusu mwelekeo wa msimu wa mvua kipindi cha Oktoba hadi Disemba mwaka amesema msimu wa mvua za vuli ni mahusiusi kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka ambayo ni Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki inayojumuisha mikoa ya Arusha, Manyara, na Kilimanjaro.
Maeneo mengine ni ya Pwani ya Kaskazini mikoa ya (Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, mikoa ya Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia, Dar es Salaam na Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba na Ukanda wa Ziwa Victoria mikoa ya Kagera, Mwanza, Geita, Shinyanga, Simiyu na Mara, pamoja na Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma (Wilaya za Kibondo na Kakonko).
“Msimu unatarajiwa kuanza kwa kuchelewa na kuambatana na mtawanyiko wa mvua usioridhisha,”Vipindi virefu zaidi ya ukavu vinatarajiwa katika mwezi Oktoba na Novemba 2022“amesema amesema Dkt. Kijazi
Hata hivyo amefafanua vipindi vya ongezeko kidogo la mvua vinatarajiwa kujitokeza katika maeneo machache hususan wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Desemba mwaka huu ambapo kwa kawaida msimu wa mvua za vuli huisha mwishoni mwa Desemb pamoja na hayo kunatarajiwa kuwepo na mwendelezo wa mvua kwa mwezi Januari mwaka huu.
Kutokana na hali hiyo Dkt. Kijazi amewashauri wakulima kupanda kwa wakati na kutumia mbegu na mazao yanayoweza kukomaa kwa muda mfupi na yanayostahimili ukame kama vile mhogo, viazi vitamu, mtama na jamii ya kunde.
Aidha amewataka wakulima kuzingatia ushauri kutoka kwa maafisa ugani juu ya kanuni Bora za kilimo ikiwa ni pamoja na kutumia mbinu na Teknolojia za kilimo himilivu za kuhifadhi maji na unyevunyevu wa udongo na uvunaji wa maji ya mvua.