Na Mwandishi Wetu.
Ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma Kwa Wateja , Leo Oktoba 4, 2023 viongozi wa Kampuni ya TIGO akiwemo Mkurugenzi Mtendaji Bwn. Kamal Okba wamewatembelea kitengo cha Huduma Kwa Wateja na kuwapongeza kwa Kazi nzuri wanayoifanya ya kuwahudumia na kuwasikiliza wateja wa Tigo masaa 24 kupitia namba 100 , Aidha viongozi hawa wamesikiliza changamoto mbalimbali zinazowasilishwa na wateja kupitia watoa huduma hawa na kuahidi kuzifanyia Kazi.
Sambamba Na hilo viongozi hawa wamewatembelea na kuwahudumia wateja wa TIGO waliokuwepo katika duka la Tigo Palm Village, tukio liliombatana na ukataji wa keki kama ishara mojawapo ya kuwashukuru kwa kuchagua kutumia mtandao wa Tigo,
Akizungumza baada ya Viongozi hawa kuyatembelea maeneo hayo muhimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma Kwa Wateja Tigo Bi. Mwangaza Matotola amesema
” Leo tumeunganika na Viongozi wetu kwa ajili ya kuwashukuru Wateja na Watoa Huduma Wetu kwa kuendelea kutuamini na kututhamini, Tulianza Wiki hii ya Huduma Kwa Wateja tukiwa Iringa na tumekua tukienda sehemu mbalimbali kuwashukuru watoa Huduma na Wateja wetu, Kwetu sisi mteja ni nguzo kubwa ya Kampuni niwatakie Heri ya Wiki ya Huduma Kwa Wateja “. Alimalizia
Naye mmoja wa Wateja Wa Tigo tuliyemkuta katika duka la Tigo Palm Village Jijini Dar Es Salaam ameipongeza kampuni ya Tigo kwa huduma nzuri na kuongezea kuwa yeye ni mmiliki wa Shule na Tigo wamempa Huduma ya Intaneti yenye kasi na Huduma ya SMS inayomrahisishia kuwasiliana na Wateja Wake.