Home Biashara TIGO WASHIRIKI MAASAI FESTIVAL 2024 NA KAMPENI YA HAKUNA MATATA KWA AJILI...

TIGO WASHIRIKI MAASAI FESTIVAL 2024 NA KAMPENI YA HAKUNA MATATA KWA AJILI YA WATALII.

MAASAI GLOBAL FESTIVAL 2024 NA TIGO : Agosti 09 & 10 , Watu walifurika katika banda la Tigo kwa nyakati tofauti tofauti pale Eden Garden – Arusha , kujipatia huduma za Kidigitali ikiwemo simu janja aina ya ZTE A34 kwa mkopo , na malipo yake ni Tsh. 650 kwa siku katika Maasai Global Festival 2024 , ambapo Kampuni ya Tigo Tanzania ilishiriki ikiwa na Kampeni yake Kabambe ya ” HAKUNA MATATA ” kwa ajili ya Watalii.

BURUDANI JUU YA BURUDANI MAASAI GLOBAL FESTIVAL 2024 : Burudani zisizo na kikomo kutoka kwa wasanii Rayvan , Barnaba , Frida Aman , Weusi na wengineo zilitikisa huku Watalii nao wakipata Burudani ” HAKUNA MATATA ” Kampeni iliyozinduliwa na Tigo yenye lengo la Kuboresha uzoefu wa Watalii na kuhakikisha wanabaki na mawasiliano ya Uhakika na ya haraka wanapozuru vivutio mbalimbali hapa nchini . 

Na Adery Masta.

Agosti , 09 – 10 Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo Tanzania imeshiriki katika Maasai Global Festival 2024 ikiwa na Kampeni yake Kabambe ya HAKUNA MATATA kwa ajili ya watalii wafikao nchini kuzuru Vivutio mbalimbali.

Akizungumza katika Tamasha hilo Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Bw. Henry Kinabo alisema 

” Kampeni ya HAKUNA MATATA inalenga kuboresha uzoefu kwa Watalii , ili kuhakikisha wanabaki na mawasiliano ya uhakika na ya haraka wanapozuru vivutio vyetu vya kitalii , Tunawaletea Vifurushi Maalum vya JAMBO PACKS ambavyo vitawapa watalii huduma bora na rahisi za mawasiliano , watalii wanapotembelea nchi yetu wanahitaji kuwa na mawasiliano bora , si tu kwa ajili ya kujuliana hali na wapendwa wao , bali pia kwa ajili ya kupata taarifa muhimu na kuendesha shughuli zao kwa urahisi “ alisema 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!