Na Adery Masta
Kampuni ya Tigo Tanzania imeendelea kudhamini Maonesho ya Biashara Arusha Maarufu kama ARUSHA TRADE FAIR yenye lengo la kutoa fursa kwa wafanyabiashara pamoja na Wajasiriamali kupata fursa ya kufanya biashara kwa pamoja hasa katika msimu huu wa sikukuu , pamoja na hayo yanatoa pia fursa kwa wananchi kupata fursa ya kufanya manunuzi yao katika eneo moja . Maonesho haya yanaendelea katika Viwanja vya Azimio la ARUSHA yameanza tangu Tarehe 12 na yataendelea mpaka Desemba , 17.
Mkaazi wa Arusha, George Mroso akipata maelezo kuhusu simu janja za mkopo kutoka wahudumu wa Tigo, katika maonesho ya biashara Arusha.
Akizungumza katika Maonesho hayo Bwn. Daniel Mainoya Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini amesemaÂ
” Kama tunavyoelewa Tigo ni Kampuni ambayo iko msitari wa mbele katika kuleta Mapinduzi ya Kidigitali Nchini , Na tupo katika maonesho haya kwasababu tunajali sana kuhusu kuwawezesha wafanyabiashara wadogo , wakati na wakubwa kwahiyo tunawakaribisha wakazi wa Mkoa wa ARUSHA na mikoa jirani kuweza kufika katika banda letu ambalo tutakua tukitoa huduma mbalimbali kama vile SIMU JANJA ZA MKOPO , TIGO PESAÂ LIPA KWA SIMU ( ambayo ni njia salama ambayo mfanya biashara anaweza tumia kufanya malipo mbalimbali )Â na TIGO BUSSINES ambayo ina solution ya huduma za Intaneti kwa wajasiriamali “
Aidha Bwn. Mainoya alimalizia kwa kuwasisitiza wateja wa Tigo kufanya miamala kwa wingi ili kuweza kujishindia zawadi mbalimbali kama vile Magari , Pesa Taslimu hadi Milioni 10 , Vifaa vya Hisense na Zawadi za Safari ya Dubai na Zanzibar kupitia kampeni yao inayotamba kwa sasa ya MAGIFTI DABO DABO