Home Michezo TIGO KUDHAMINI BONANZA LA NYERERE DAY MUSOMA MJINI, WADAU WENGINE WAITWA

TIGO KUDHAMINI BONANZA LA NYERERE DAY MUSOMA MJINI, WADAU WENGINE WAITWA

Na Shomari Binda-Musoma

KAMPUNI ya mtandao wa simu ya mkononi ya Tigo mkoa wa Mara imedhamini sehemu ya kufanikisha bonanza la michezo ya Nyerere Day.

Bonanza hilo litafanyika kwa siku 2 oktoba 13 na 14 mjini Musoma kwa kushirikisha timu za veteran kutoka kanda ya ziwa.

Timu 7 tayari zimethibitisha kushiriki bonanza hilo zikiwe za Simiyu veteran,Mwanza veteran, Rocky City veteran,Kishapu veteran,Musoma veteran,Mara veteran na Biashara United veteran.

Mmoja wa waratibu wa bonanza hilo Katunzi Kiza amesema wanaishukuru kampuni ya Tigo kwa kuamua kuwashika mkono ili kufanikisha bonanza hilo.

Amesema bonanza hilo ikiwa ni kumbukizi ya miaka 24 ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere litakuwa na wanamichezo wengi hivyo bado wanahitaji wadau wa kuwashika mkono.

Licha ya Tigo,Katunzi amewataja wadau wengine ambao wameonyesha kuwaunga mkono kuwa ni Eyembe Platinum,TTCL,Dream Garden Resort,CRDB Benk,mganga mkuu wa manispaa ya Musoma,Royal Polyclinick,Amref na NHIF Mara.

“Tunawashukuru Tigo na wadau wengine kwa kujitokeza kudhamini bonanza hili ambalo litashirikisha timu kutoka kanda ya ziwa”

“Kwa kuwa tutakuwa na wageni wengi bado tunawaomba wadau wengine kujitokeza kudhamini bonanza hili ili liweze kufanikiwa”, amesema Katunzi.

Katika kujiandaa na bonanza hilo kocha wa timu ya Musoma veteran Ramadhan Magoye amesema kama wenyeji wamejiandaa vizuri na timu yao pamoja na kuwapokea wageni watakaokuja kushiriki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!