Home Michezo TIGO KILI HALF MARATHON 2024 YAZINDULIWA RASMI, TIGO WAONGEZA ZAWADI KWA WASHINDI

TIGO KILI HALF MARATHON 2024 YAZINDULIWA RASMI, TIGO WAONGEZA ZAWADI KWA WASHINDI

Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Tigo, Woinde Shisael amesema Tigo inajivunia kuwa mmoja wa wadhamini wa Mbio za kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathon kwa mwaka 2023 kwani mbio hizo huitangaza Tanzania kwa kuwakutanisha washiriki zaidi ya 12,000 kutoka nchi takribani 55, na kupelekea kukuza vipaji na uchumi wa Taifa.

Woinde ameyasema hayo Oktoba 20, 2023 wakati wa uzinduzi wa mbio hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika Februari 25, 2024 ikiwa ni toleo la 22 tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.

“Kama kampuni ya mawasiliano, tumekuwa wadhamini wa Tigo Kili Half Marathon kwa mwaka wa 9 sasa kutokana na ukweli mashindano haya yamekuwa ni jukwaa muhimu katika kukuza vipaji, uchumi wa taifa pamoja na uhifadhi wa mazingira hususan maeneo ya Mlima Kilimanjaro”

Woinde amesema mashindano hayo yanaendelea kukua kila mwaka huku yakiteka hisia za washiriki wengi wakiwemo wanariadha mahiri wa kimataifa kutoka sehemu mbalimbali duniani.

“ Sisi kama kampuni ya TIGO tunajiweka karibu na watu pamoja na kurudisha kwa jamii na ndio maana mmekua mkituona tukidhamini Mambo mengi mbalimbali yanayowalenga watu  , katika mbio hizi tumekua tukitumia njia ya kujisajili kupitia simu zetu za mkononi yaani Tigo Pesa Lipa Kwa Simu Pamoja Na website Yetu ivyo kurahisisha zoezi la washiriki kujisajili,  Kwahiyo tunawasihi washiriki kuanza kujisajili mapema na Kwa Upande wa Zawadi tumeongeza kiwango kutoka Dola 6000 hadi Dola 10000 hii itaongeza hamasa kwa wakimbiaji na italeta watu wengi kushiriki Tigo Kili Half Marathon  2024 , Karibuni sana katika mbio hizi muweze pia kushuhudia matumizi ya Intaneti yetu ya kasi ya 5G itakayokuunganisha na ndugu,  jamaa na Marafiki kwa kipindi chote cha mbio hizi ,” alisema.

kwa upande Meneja Mkaguzi wa Ndani kutoka Bodi ya Utalii Tanzania ( TTB)  Bwn.  Steven Mpeta , amesema mbio za Kilimanjaro Marathon zimeendelea kutoa mchango mkubwa katika kukuza sekta ya utalii kwa kupitia utalii wa michezo na hivyo kuungana na Serikali katika kukuza sekta ya utalii nchini.

“Nawapongeza wadhamini wote wakiongozwa na mdhamini mkuu Kilimanjaro Premium Lager, Tigo -21km Half Marathon Kwa mchango wenu mkubwa, bila nyinyi na wafadhili wengine wote pamoja na washiriki, mafanikio haya yasingeonekana”

Aidha Bwn.  Mpeta ametoa wito kwa washiriki Watanzania kujiandaa na mashindano hayo ya kimataifa ili kuhakikisha zawadi nyingi zinabaki nyumbani lakini pia amewataka washiriki na mashabiki kutumia msimu wa Marathon kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii miongoni mwao vikiwemo Mlima Kilimanjaro.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!