Home Kitaifa TIC YATOA SEMINA JUU YA UWEKEZAJI WA WAZAWA MKOANI MARA

TIC YATOA SEMINA JUU YA UWEKEZAJI WA WAZAWA MKOANI MARA

Na Shomari Binda-Musoma

KITUO cha Uwekezaji Tanzania ( TIC) kimeendesha semina kwa wafanyabiashara mkoani Mara juu ya kuwa wawekezaji na kupata fursa zikiwemo unafuu wa kodi.

Semina hiyo iliyofanyika leo julai 23 kwenye ukumbi wa uwekezaji imefunguliwa na mkuu wa mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi na kusisitiza wafanyabiashara kuja kuwekeza mkoani Mara.

Katika hotuba yake ya ufunguzi Mtambi amesema mkoa wa Mara unazo fursa nyingi za uwekezaji nchi kavu na majini na ni sehemu salama ya kuwekeza.

Amesema asilimia zaidi ya 70 ya hifadhi ya Serengeti ipo mkoani Mara hivyo kuna nafasi kubwa ya kufanya uwekezaji wa kitalii.

Kanali Mtambi amesema licha ya eneo la nchi kavu lipo ziwa victoria ambapo unaweza kufanyika utalii wa majini na shughuli za uvuvi ukiwemo wa vizimba.

” Tunawakaribisha sana kituo cha uwekezaji mkoani Mara kutoa semina kwa wafanyabiashara wetu ili nao wawe wawekezaji kwenye nchi yao.

” Mkoa wa Mara zipo fursa nyingi za kufanya uwekezaji kikubwa ni wafanyabiashara kupewa elimu juu ya manufaa ya kufanya uwekezaji “,amesema.

Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania ( TIC) Gilead Teri kwenye taarifa yake iliyotolewa na Afisa Uhamasishaji wa kituo hicho Felix John amesema upo unafuu mkubwa kwa wawekezaji wa ndaini ikiwa ni pamoja na masuala ya kodi.

Amesema hii ni kampeni maalumu ya kuwahamasisha watanzania kushiriki na kuziona fursa za uwekezaji na kufanya uwekezaji ili kujiinua kiuchumi.

Mkurugenzi huyo amesema kituo cha uwekezaji kinayo majukumu mengi ikiwemo kuratibu na kuhamasisha uwekezaji kwa wananchi.

Mmoja wa washiriki wa semina hiyo Boniphace Ndengo ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya HAIPPA PLC Tanzania Limited ameishukuru TIC kwa elimu waliyoitoa kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Mara.

Amesema semina waliyoitoa itawasaidia wafanyabiashara kujua faida za uwekezaji na kuamua kuwekeza kwaajili ya kujiinua kiuchumi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!