Home Kitaifa TGNP YATOA MAFUNZO YA UFEMINIA NGAZI YA JAMII VITUO VYA TAARIFA NA...

TGNP YATOA MAFUNZO YA UFEMINIA NGAZI YA JAMII VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA WILAYA YA SAME MKOANI KILIMANJARO

Na Ashrack Miraji Same kilimanjaro

Mwezeshaji ngazi ya jamii kutoka TGNP Stella John Amesema mafunzo hayo yanayotolewa kwa vituo vya taarifa na Maarifa yanalenga kutoa Elimu kwa jamii kuhusu ukatili wa kijinsi na kukemea vitendo viovu vilivyo kinyume na maadili kwa jamii ikiwemo ukeketaji, mfumo dume na Ulawiti.

Aidha amehimiza wana vikundi wote wa taarifa na Maarifa (KC) Mkoani kilimanjaro kuendelea kufanya kazi ya kukusanya taarifa Mbalimbali dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na kufikisha mahali husika ili hatua zichukuliwe kwa haraka pia kushirikiana kwa pamoja kufuatilia miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali kwenye maeneo yao.

Mmoja wa wajumbe wa kikundi cha Taarifa na Maarifa (KC) kata ya Rugulu wilayani Same Happiness Turira miongoni mwa wanufaika wa mafunzo hayo ameshukuruTNGP kwa kuendelea kuwajengea uwezo wa kujitambua kifikra na kuvunja ukimya Katika kutoa Elimu Sehemu Mbalimbali kuhusu Ukatili wa kijinsia kwenye shule na vikundi vya vikoba na kwenye mikutano ya hadhara.

“Mafunzo kama haya yanatujengea uwezo wa kujiamini na kutatua migogoro na kukemea ukatili kwenye taifa letu, kwa niaba ya washiriki wenzangu nishukuru TGNP kuendelea kutupatia mafunzo ya aina hii kwakua yanazidi kutuimarisha namna ya kufuatilia taarifa mbalimbali kwenye maeneo yetu”. Alisema.

“Pamoja na hayo TNGP imeendelea kutujengea uaminifu hasa wakina mama kujiamini katika kulinda familia zetu na jamii husika kwa kutujengea uwezo sisi kuwa viongozi wa kubwa baadae na kuendelea kulitumikia taifa letu kama tunavyomuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani alivyo jasiri na mchapakazi hodari na sisi kama vikundi vya kutoa taarifa na Maarifa kwa jamii inayotuzunguka tuendelee kushirikiana na Serikali kwa pamoja kudhibiti na kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia Mkoa wa kilimanjaro”.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!