Home Kitaifa TGNP WAJADILI NA KUTATHIMINI BAJETI NA MPANGO WA SERIKALI KATIKA JICHO LA...

TGNP WAJADILI NA KUTATHIMINI BAJETI NA MPANGO WA SERIKALI KATIKA JICHO LA KIJINSIA

Mwenyekiti wa Bodi Mwenyekiti wa bodi ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) akiongea wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Kijiwe cha Kahawa leo Alhamis Juni 13, 2024 katika ofisi za TGNP, Mabibo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) akiongea wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Kijiwe cha Kahawa leo Alhamis Juni 13, 2024 katika ofisi za TGNP, Mabibo jijini Dar es Salaam.
Washiriki mbalimbali wa Kijiwe cha Kahawa wakifuatilia hotuba ya taarifa ya hali ya uchumi wa nchi kwa mwaka 2023 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2024/2025 iliyowasilishwa leo Juni 13, 2024 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mhe. Profesa Kitila Mkumbo

Kwa takribani miaka nane (08) sasa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umekuwa na kawaida ya kuwa na majukwaa mbalimbali ikiwemo jukwaa lijulikanalo kwa jina la Kijiwe cha Kahawa kwa lengo la kujenga nguvu za pamoja ili kuleta chachu ya mabadiliko chanya kisera, kiutendaji na kifikra.

Hayo yamesemwa leo Alhamis Juni 13, 2024 na Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali akiongea katika ufunguzi wa jukwaa hilo ambapo amesema, jukwaa hilo limefanikiwa kuwaleta pamoja wadau mbalimbali na kutoa fursa ya kusikiliza hotuba ya hali halisi ya uchumi pamoja na ikiwa ni pamoja na kutathimini bajeti kuu ya serikali 2024 /2025 kwa mtazamo wa jinsia kwa kuzingatia matarajio ya wananchi.

Mwenyekiti huyo wa bodi ameendelea kwa kusema kuwa, jukwaa hilo inatumika pia kama nyenzo ya kuwakutanisha wadau kwa ajili ya kuunganisha nguvu za pamoja katika kudai utengaji wa bajeti kwa mlengo wa kijinsia ambapo nguvu hizo zimeanza kuzaa matunda.

Moja ya hatua zilizopigwa ni pamoja na uingizwaji wa bajeti za kijinsia katika malengo matatu ya kimkakati kati ya malengo matano yaliyopo kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo” alisema Bi. Akilimali na kuongeza

Licha ya kuwepo kwa mafanikio bado kuna changamoto ikiwemo utengwaji hafifu wa rasilimali zinazoweza kuchangia kufikia usawa wa kijinsia. Bado hatujaweza vya kutosha kuingiza masuala ya kijinsia kwenye sheria na sera hii ni kutokana kukosekana mpango mzuri na uratibu kutoka Wizara ya Fedha

Amezitaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja utolewaji wa rasilimali fedha aidha kidogo au nje ya muda jambo ambalo linachangia kufifisha azma ya kufikia usawa wa kijinsia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji
wa TGNP, Lilian Liundi amesema, bajeti kuu ya serikali ya mwaka 2024/2025 imekuja katika muktadha wa kipekee katika kipindi ambacho nchi tunatengeneza dira ya Taifa ambayo itaamua hatma ya maisha yetu ya miaka 25 ijayo.

Kuhusu umuhimu wa ushiriki wa wananchi katika michakato ya bajeti Liundi amesema

Bajeti ni kitu cha muhimu sana, na ni lazima wananchi watoe maoni na sauti zao. Kufuatia hilo, TGNP tumeandaa jukwaa hili (Kijiwe cha Kahawa) tukifahamu umuhimu wa ushiriki wa wananchi katika michakato ya bajeti kwa kuwa bajeti inatoa dira ya mwaka ya maisha ya watu. Tunatamani wananachi washiriki michakato yote hiyo”

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji huyo ametoa rai kwa serikali kuangalia suala la utoshelevu wa rasilimali zote ambazo zitawawezesha wanawake wengi kushiriki katika uchaguzi ili waweze kutoa sauti zao kupitia uwakilishi wao kwenye nafasi mbalimbali za uongozi kinyume na sasa ambapo takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wanawake katika nafasi za uongozi ngazi za serikali za mitaa kuwa ni ndogo.

Wakiongea kwa nyakati tofauti, Hellen Sisya ambaye ni Mtendaji Mkuu wa taasisi ya Her Education Foundation na Christina Silas kutoka Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) wamesema matarajio yao ni kuona bajeti ya mwaka 2024/2025 inaleta unafuu kwa vijana na makundi maalumu pamoja na kuweka mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ili kuelekea kwenye utekelezaji wa bajeti hiyo zikijitokeza changamoto zozote kutokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi basi zisiathiri uchumi wa Taifa.

Dhima ya Kijiwe cha Kahawa mwaka huu inasema ” Kuelekea Bajeti Kuu ya Serikali 2024 /2025, Wekeza katika Usawa wa Kijinsia, Ushiriki wa Wanawake katika Uongozi na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayogusa makundi yote”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!