Home Kitaifa TFS TOENI ELIMU YA UMUHIMU WA UPANDAJI MITI – NDARUKE

TFS TOENI ELIMU YA UMUHIMU WA UPANDAJI MITI – NDARUKE

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kibiti mkoani Pwani Juma Ndaruke amewataka Wakala wa Misitu Tanzania – TFS kutoe elimu ya umuhimu wa upandaji miti kwa jamii ili wahamasike kupanda miti zaidi ya ilivyosasa wilayani humo.

Amesema hayo wakati kamati ya siasa ya wilaya ya Kibiti ilipofanya ziara za kutembelea shughuli mbalimbali zinazofanywa na TFS wilaya ya Kibiti amesema TFS waendelee kutoa elimu kwa jamii ili iwe rafiki na kusaidia upandaji mti wilayani humo.

Alisema katika elimu watakayotoa kwa wananchi pia wahamasishe na upandaji wa miti ya matunda, miti ya vivuli na miti ya mbao ili miche inayotolewa na TFS ipandwe kwa wingi na lengo la serikali litimie kwa jamii.

Ndaruke alisema wananchi wa wilaya ya Kibiti wanapenda zaidi kupanda upandaji wa miti ya matunda na miti ya vivuli hivyo hamasa zaidiu kwa wananchi inahitajika ili kuongeza kasi ya uzalishaji wa miche ya matunda na miti ya vivuli.

Aidha Mwenyekiti huyo aliwataka TFS waelimishe wananchi hata waifanye TFS ni rafiki na msaada na waambie wananchi kuhusu fulsa mbalimbali zilizopo katika ufugaji nyuki ili wafuge na wanufaike kupitia ufugaji nyuki.

“Kuna fursa katika ufugaji nyuki na wananchi wanatakiwa kujua fulsa hizo waambiwe waanze ufugaji wanufaike fanyeni mikutano wazi mkiwaaambia wananchi kuhusu fulsa hizo kwa kujikwamua kiuchumi kupitia sekta ya ufugaji nyuki” alisema Ndaruke.

“Huku kwetu misitu ipo mingi hivyo ni rahisi kufanya ufugaji nyuki Wakieliemishwa vizuri” alisema Ndaruke.

Muhifadhi Mkuu wa Wakala huduma za misitu wa wilaya Devis Mlowe amesema mwaka jana walipanda miche laki 5 ya miti ya matunda, vivuli na miti ya mbao na kwa mwaka uliopita walipanda miche 434000 ambayo ilipandwa kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali wakiwemo taasisi za serikali, wananchi, taasisi za dini na taasisi binafsi pamoja na wilaya jirani ya Mkuranga, Rufiji, Kibaha sambamba na kupanda miti katika maeneo ya hifadhi.

Kwa upande wa ufugaji Nyuki Mlowe amesema katika wilaya nzima ya Kibiti wana mizinga 124 ya nyuki wanaouma imewekwa kwenye maeneo ya Kibiti mjini, ya hifadhi ya Mchungu na kwenye eneo la hifadhi ya misitu ya huko Delta Nyamisati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!