Home Kitaifa TenMeT WAZINDUA MPANGO MKAKATI WA 2023-2027 KULETA MAPINDUZI YA UCHUMI

TenMeT WAZINDUA MPANGO MKAKATI WA 2023-2027 KULETA MAPINDUZI YA UCHUMI

Na Magrethy Katengu

Wadau wa sekta ya Elimu wameshauriwa licha ya harakati zao za kuboresha elimu nchini pia wasaidie wanafunzi katika suala la Maadili huko shuleni kwani hali ya tabia za baadhi ya watoto zimebadilika na Mwalimu hawezi peke yake..

Ushauri huo umetolewa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Udhibiti Ubora wa Elimu Tanzania Wizara ya Sayansi na Teknolojia Ephraim Simbeye katika uzinduzi wa Iboreshwaji mpango Mkatati sekta ya Elimu mwaka 2023 JanuariHadi 2027 Desemba ulioandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TenMeT) licha ya jitihada wanazozifanya kuchangia mahitaji wanafunzi wanaotokea kaya masikini lakini pia waangalie namna ya kuwasaidia wanafunzi kwani Maadili yameporomoka Mashuleni ikilinganishwa miaka ya hapo awali

“Msaidie eneo la maadilo Shuleni hali ni hairidhishi maadili yameporomoka shule zetu zinazidi kwenda kombo Waalimu kutokana na wingi wa wanafunzi kuwasaidia peke yao kwa kuwa nyie mko karibu nao majumbani muda mwingi ni vyema mkasaidia hili Ili kusaidia kuleta kizazi chenye maadili mema” amesema Mkurugenzi

Sembeye amesema kuwa serikali imekuwa ikifanya mabadiliko ya sera ya Elimu kwa kuzingatia mabadiliko katika sekta ya ajira kwa kushirikiana na asasi za kiraia na Asasi nyingine kuweka vipaumbele katika masuala ya ukatili wa kijinsia ikiwa na lengo la kuleta usawa Kwa Jamii

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya wa mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT)Faraja Nyalandu amesema kuwa kutokana nakuwepo kwa Janga la Uviko 19 kumeleta changamoto ya kujifunza kwa watoto hali inayochangia kushusha morali ya watoto kujifunza hivyo kupitia mpango mkakati na mapendekezo waliyoyatoa utaleta mabadiliko ya sera ya Elimu kutaleta chachu ya Teknolojia sekta ya Elimu.

Naye Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania(TenMeT)Ochola Wayoga amesema huo Mpango mkakati uliozinduliwa unakwenda kugusa maisha ya vijana kuanzia ngazi ya za Elimu darasa la kwanza Hadi vyuo vikuu kwa kuwasaidia kimaadili kuweza kujitawala na utachangia katika ongezeko la pato la Taifa kwa kuwafanya wawe wabunifu.

Aidha Mtandao wa Elimu Tanzania unamitiza miaka 23 tangu kuanzishwa kwake 1999 na umekuwa ikifanya shughuli zake kwa kugusa Jamii katika Mikoa mbalimbali hapa nchi hivyo leo wakizindua Wakizindua Mpango mkakati wamekata keki ya pamoja na kusherekea siku hii ya kumbukumbu kwao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!