Na Boniface Gideon -TANGA
Taasisi ya Wanafunzi wa meno Tanzania ‘TDSA’,imesema kwasasa imeamua kutambulisha mfuko mpya wa lugha za utoaji wa huduma zinazojulikana kama ‘Afya Jumuishi’, ikiwa na lengo kuu lakupungaza matatizo ya kinywa Nchini,
Aidha TDSA imesema matatizo ya kinywa na meno Nchini yanazidi kuongezeka ambapo imefikia zaidi ya asilimia 60.
Rais wa TDSA aliyemaliza muda wake ,Yona Musa aliwaeleza Waandishi wa Habari mwishoni mwa wiki kando ya mkutano Mkuu wa kitaaluma kati ya TDSA na Wataalamu wa Afya,Watunga Sera na wadau wa Afya,mitindo ya maisha imechangia kusababisha matatizo ya kinywa na meno Nchini kuzidi kuongezeka kila siku,
“matumizi yakupindukia ya vyakula vyenye sukari nyingi husababisha kuoza na kutoboka kwa meno, lakini pia usafi wa kinywa bado ni tatizo,kwakawaida tunamshauri mtu apige mswaki angalau mara mbili kwa siku,asubuhi baada ya kunywa chai na usiku baada ya kula, lakini pia tunamshauri mtu apunguze matumizi ya sukari nyingi kwakuwa inaozesha meno” Alieleza Yona
Alisema baada ya kuona tatizo hilo likizidi kuongezeka,TDSA imelazimika kuja na sera mpya inayoitwa ‘Afya Jumuishi’,inayolenga kumsaidia mgonjwa kutibiwa na Wataalamu mbalimbali wa Afya huku akipatiwa Elimu ya namna ya Kutunza kinywa,
“kupitia sera yetu mpya, mgonjwa atapata huduma kutoka kwa wataalamu mbalimbali wa Afya,lengo ni kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma, tunataka mgonjwa asitibiwe kiuongo kimoja bali apate huduma za mwili mzima,na hii ndio mana halisi ya ‘Afya Jumuishi’,kwakufanya hivyo tutakuwa tumemsaidia mgonjwa kupata huduma nzuri zaidi”Aliongeza Yona
Aliwataka Wananchi kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi huku, pamoja na kuzingatia usafi wa kinywa,
“matumizi ya bidhaa zenye sukari nyingi pamoja na kushindwa kuzingatia usafi wa kinywa unaongeza hatari ya kupata matatizo ya kinywa na meno, kwahiyo kila mmoja wetu ajitahidi kuzingatia ushauri wa kitaalamu ili kuondoa hatari ya kupata matatizo ya kinywa na meno” Aliongeza Yona
MWISHO