Mkuu wa Wilaya ya Singinda Mhe. Godwin Gondwe ( kushoto ) katika banda la TBS lililopo katika Maonesho ya saba ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayofanyika katika viwanja vya Bombadier Mkoani Singida, Ikumbukwe Maonesho haya yalifunguliwa rasmi Septemba , 10 , 2024 mkoani Singida na Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi, ambapo katika hotuba yake alisisitiza umuhimu wa elimu ya kujitegemea huku akiwahimiza wananchi kujitokeza kujifunza kupitia maonesho hayo ili kujikwamua kiuchumi.
Na Mwandishi Wetu.
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendela kutoa elimu ya ubora wa bidhaa katika Maonesho ya saba ya Mifuko na Programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayoendelea katika viwanja vya Bombadier mkoani Singida.
Akizungumza katika Maonesho hayo ambayo yameanza Septemba 8, 2024 na yanatarajiwa kumalizika Septemba 14, 2024, Afisa Mtoa Elimu TBS Bw. Sileja Lushibika amesema TBS imeshiriki na kutoa elimu kwa wajasririamali pamoja na wageni waliofika katika banda lao juu ya uwezeshaji wananchi kiuchumi pamoja na umuhimu wa kuwa na alama ya ubora ya TBS katika bidhaa.
Ushiriki wa TBS katika maonesho haya unaonyesha wazi dhamira yake ya kuunga mkono juhudi za kiuchumi za wananchi na kutoa mchango wa kipekee katika maendeleo ya sekta ya viwanda na biashara nchini Tanzania.
.